Naibu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mh. Anthony
Mavunde leo amezindua programu ya Urasimishaji Ujuzi kwa Vijana ambao
wana ujuzi lakini hawakupitia katika mfumo rasmi wa mafunzo ya
Ufundi(Recognition of Prior Learning).
Ufunguzi
huo wa Program hii ya Urasimishaji Ujuzi ambao unagharamikiwa na Ofisi
ya Waziri Mkuu umefanyika leo katika Chuo cha VETA Jijijni Tanga na
kujumisha jumla ya Vijana 701 kutoka mikoa ya Tanga,Kilimanjaro,Arusha
na Manyara wanatarajiwa kunufaika na mpango huo.
Akizungumza
na Vijana hao, Mh.Mavunde amesema serikali inatekeleza mpango mkubwa wa
ukuzaji ujuzi kwa Vijana unaolenga kuwafikia takribani Vijana Milioni 4
nchi nzima kwa lengo la kuwajengea ujuzi stahiki utakaowasaidia kupata
Ajira na kujiajiri wenyewe.
Aidha
Naibu Waziri Mavunde amewataka Vijana wote kuchangamkia fursa
mbalimbali zitokanazo na ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka
Hoima,Uganda-Tanga ambapo serikali kuu na serikali ya Mkoa wameendelea
kujenga mazingira rafiki ya kuhakikisha Vijana wanafikia malengo yao.
Wakizungumza
baada ya kuzinduliwa program hiyo, Vijana hao wameishukuru Serikali kwa
Mpango huu wa urasimishaji ujuzi ambao unawapa fursa ya kupewa cheti
cha Ufundi kutoka VETA bila kupitia utaratibu wa kawaida wa masomo
ambapo takribani Vijana 3900 watanufaika na Mpango huu nchi nzima.
No comments:
Post a Comment