Mkuu wa Idara ya ustawi wa Jamii Manispaa ya Ilala Francisca francis Makoye Akizungumza na viongozi wa Madhehebu ya kutoka kata 40 za Manispaa ya Ilala walifika katika mkutano huo, aliye upande wa kushoto ni Mwenyekiti wa muda wa mkutano huo Sheikh Hamisi Mohamed (Picha na John Luhende.)
Na. John Luhende
Mwambawahabari
Viongozi wa madhehebu ya Dini katika manispaa ya Ilala wamepatiwa mafunzo pamoja na kufanya majadiliano kuhusu mchango wao katika katika mwitikio wa masuala yanayo husu UKIMWI ,kwakuwa wao hukutana na watu wa jaamii zote ili waweze kuwaeleza na kuwa kumbusha waumini waoku jiepusha na ugonjwa huo.
Baadhi ya viongozi wa madhehebu ya Dini kutoka kata mbalimbali za Manispaa ya Ilala walio hudumia mkutano huo wakimsikiliza mwezeshaji kwa makini hayupo picha ni (Picha zote na John Luhende.)
Akizungumza katika ufunguzi wa
mkutano huo, mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii usatawi wa jamii Manispaa ya
Ilala Francisca Francis Makoye, Amewaeleza
viongozi hao kuwa haliya
maambukizi ya UKIMWI katika manispaa hiyo
kuwa sinzuri na wao kama viongozi wa Dini wanao wajibu wa kuwakumbusha waumini
wao kuwa waamifu kwa ndoa zao na vijana kujitunza, na kuaachana na
ngono uzembe, kusubiri muda wao japo kuna changamoto nyingi katika umri wao.
Baadhi ya viongozi wa madhehebu ya Dini
kutoka kata mbalimbali za Manispaa ya Ilala walio hudumia mkutano huo wakimsikiliza mwezeshaji kwa makini hayupo picha ni (Picha zote na John Luhende.)
Aidha amewakumbusha vijana kutumia
vizuri ujana wao na kushinda vishawishi ili kujiepusha na ngono ambayo
imeelezwa kuwa ndiyo njia kuu inayo
eneza ugojnwa huo ukilinganisha na njia zingine.
Hata hivo amesema kamati za kata za kudhibiti UKIMWI , moja wapo ya majukumu yake ni kupanga na
kushirikiana na wananchi na wadau wengine kuhusu mipango ya kupambana na
maambukizi, kukuza uelewa wa
wananchi kuhusu UKIMWI na uwezo wa
kiuchumi wa waathiriwa.
Pamoja na hayo ameongeza kuwa juhudi zinahitajika kwa kila kiongozi na
wanachi kwa ujumla katika kupambana na janga la UKIMWI katika ngazi ya kata ili hatimaye
malengo ya 90 90 90ifikapo 2020 ambayo ni asilimia 90 ya WAVIU wana jua haqli
ya kuishi na VVU, na asilimia 90 ya waliogundulika na VVU wanapata matibabu
ndelevu ya dawa za kufubaza virusi na
asilimia 90 ya watu wote wanapata dawa za kufubaza Virusi watakuwa na kiwango
kidogo cha Virusi.
Naobaadhi ya viongozi walishiriki
mkutano huo wameishukuru manispaa hiyo kwa kuandaa mkutano huo kwani umewaogezea
uelewa juu ya afya zao na waumininwao , Shekh Indrisa kutoka Majohe ni moja ya
viongozi hao, ameishukuru Manispaa ya Ilala kwa kuandaa mkutano huo wa siku mbili kwani wameweza
kuelewa namna serikali inavyo wajali
wanachi wake hasa katika kuwa hudumia kwa kuwapatia dawa na
hudumanyingine za kiafya na kuhakikisha usalama wao wakati wote.
“kwakweli kuna jambo moja sizuri sana
hasa wawezeshaji walivyo tuelezea kuhusu sheria ya UKIMWI ya 2008 kuhusu watu
wanaoeneza ugojwa huu kwa makusudi, naomba watu hao waache kabisa kwa mwenyezi
Mungu atawapa hukumu kwa kuwauwa wenzaokwa makusudi” Aalisema shekh huyo.
No comments:
Post a Comment