Ofisa Mtendaji Mkuu wa Tume ya Uchaguzi
na Mipaka Kenya ‘IEBC’, Ezra Chiloba ametangaza kuachia ngazi leo huku wafuasi
wa Muungano wa Upinzani (NASA) wakifanya maandamano katika baadhi ya maeneo
nchini humo kushinikiza kuondolewa kwa maafisa 12 wa tume hiyo akiwemo Ofisa
huyo kwa shutuma za kuvuruga uchaguzi wa Agosti 8, mwaka huu.
Maandamano hayo yaliyotawaliwa na ghasia
katika baadhi ya maeneo ni mwitikio wa wito uliotolewa jana na Kiongozi wa
Upinzani, Raila Odinga aliyewataka wafuasi wake kujitokza kwa wingi kuandamana
hadi Makao Makuu ya IEBC, ikiwa ni siku chache tu zimepita tangu Mahakama ya
Juu Kenya kufutilia mbali matokeo ya urais yaliyompa ushindi Rais Kenyatta.
Wafuasi wa NASA walikuwa wakimshutumu
Chiloba na watendaji wengine kufanya njama za kuingilia mchakato wa uchaguzi
huo na kumsaidia Rais Kenyatta kuibuka kidedea.
Waandamanaji hao wamebeba matawi ya miti,
mabango, huku wakipiga mayowe na honi za pikipiki kuanzia barabara ya Obote, kisha
mtaa wa Oginga Odinga kabla ya kuchukua barabara kuu ya Kenyatta hadi Mtaa wa
Ang’awa katikati ya Jiji la Nairobi huku watu wachache wakiwa wametiwa nguvuni
na Jeshi la Polisi.
Haya yanajiri ikiwa ni siku 30 tu zimesalia hadi kufanyika uchaguzi wa marudio, Oktoba 26, mwaka huu
No comments:
Post a Comment