MAHAKAMA Kuu Kanda ya Sumbawanga mkoani
Rukwa imewahukumu adhabu ya kifo watu sita ambao ni ndugu wakazi wa Kalambo
baada ya kupatikana hatia ya kumuua ndugu yao.
Ndugu hao wamedaiwa kwamba walifikia
uamuzi wa kumuua ndugu yao huyo kwa madai ya kwamba anajihusisha vitendo vya
kishirikiana.
Hukumu hiyo imetolewa leo Jumanne na Jaji
Mahakama hiyo, Dk Adam Mambi baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa
mahakamani hapo na upande wa mashitaka uliopeleka mashahidi sita ili
kuthibitisha mashitaka hayo.
Waliokutwa na hatia katika shauri hilo ni Ferdinand Kamande, Peter Mpandisharo, Edes Kamande, Stephen Sikanda, Henrick Nguvumali na Anatory Kamande huku Alistid Kamande na Will broad Kamande wakiachiwa huru kwa kutokutwa na hatia.
No comments:
Post a Comment