Wednesday, September 6, 2017

WADAU WA PAMBA MKOANI SIMIYU WAKUTANA KUJADILI MSTAKABALI WA ZAO LA PAMBA

Wadau wa zao la pamba mkoani Simiyu wamekutana na kufanya kikao lengo likiwa ni kujadili masuala mbalimbali yanayohusu mstakabali wa zao hilo kuelekea katika kipindi cha msimu wa kilimo kwa mwaka 2017/2018.

Kikao hicho kimewahusisha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wenyeviti wa Halmashauri, Maafisa Kilimo, Wamiliki na wataalam wa Makampuni ya Ununuzi wa Pamba kutoka ndani ya nje ya Mkoa wa Simiyu ambacho kiliongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka.

Akifungua kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Simiyu amesema Mkoa huo unazalisha zaidi ya asilimia 55 ya pamba yote hapa nchini, hivyo akawataka wadau wa pamba mkoani humo kutumia vema kikao hicho kujadili kwa umakini masuala muhimu katika sekta ya pamba ili wananchi waweze kuzalisha kwa tija na kunufaika na zao hilo.

 Katika kikao hicho Wadau wa zao la pamba wamekubaliana kuwa kilimo cha mkataba kwa wakulima kiwe cha hiari sio lazima na elimu indelee kutolewa kwa wakulima na wanunuzi wa pamba kuona namna wanavyoweza kutumia kilimo cha mkataba kuongeza tija katika uzalishaji kwa wakulima watakao kuwa tayari.

Akichangia hoja katika kikao hicho Afisa Kilimo Halmashauri ya Wilaya Bariadi, Martha Zongo, amesema kilimo mkataba kikifanyika kwa makubaliano yatakayowekwa baina ya wakulima walio tayari  na makampuni yanayonunua pamba, wakulima wasio na uwezo watapata pembejeo na huduma za ugani kutoka kwa wataalam wa Makampuni hayo na kuongeza uzalishaji maana katika baadhi ya maeneo kuna upungufu wa maafisa Ugani.


Kuhusu suala la matumizi ya mbegu wadau walikubaliana kuwa wananchi wa Mkoa wa Simiyu watapata mbegu zenye manyoya na zisizo na manyoya kama ilivyoelezwa na Bodi ya Pamba na ni hiari yao kuchagua mbegu watakayoitaka, hivyo elimu iendelee kutolewa kwa wakulima juu ya matumizi ya mbegu hizo ili waelewe mbegu iliyo bora zaidi kwa uzalishaji wenye tija.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Fabian Manoza amependekeza Taasisi ya Ukaguzi na Uthibitisho wa Mbegu Nchini(TOSCI) waone umuhimu wa kufungua tawi Kanda ya Ziwa ili kufuatilia kwa ukaribu udhibiti wa mbegu za pamba na Wakala wa Mbegu (ASA) watafute mashamba pia katikakanda hii ili waweze kuzalisha mbegu kwa lengo la kurahisisha upatikanaji wa mbegu bora za pamba.

Vile vile katika suala la mbegu Bw. Stephen Lawrence kutoka Kampuni ya Nyanza Cotton  inayojishughulisha na ununuzi wa Pamba akiungwa mkono na wadau wengine, aliomba Serikali itoe ruzuku kwa wakulima ili waweze kumudu gharama za ununuzi wa mbegu.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu aliwahakikishia wajumbe kuwa mapendekezo na maazimio yaliyotolewa katika kikao hicho atayawasilisha katika Kikao cha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Kasim Majaliwa na Wakuu wa Mikoa inayolima pamba hapa nchini kitakachofanyika Mjini Dodoma, tarehe 08/09/2017.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(katikati) akizungumza na wadau wa zao la pamba Mkoani humo(hawapo pichani) katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi ili kujadili suala la Kilimo cha Pamba mkoani hapo(kushoto) Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga na (kulia) Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe.Dkt.Titus Kamani.
Baadhi ya wadau wa zao la pambaMkoani Simiyu wakifuatilia hoja mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi ili kujadili suala la Kilimo cha Pamba mkoani hapo.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe.Dkt.Titus Kamani akichangia hoja katika kikao cha Wadau wa pamba Mkoani humo kilichofanyika Mjini Bariadi lengo likiwa ni kujadili mstakabali wa zao hilo mkoani humo.
Bi.Suzan Mollel kutoka katika Kampuni ya OLAM inayojishughulisha na ununuzi wa pamba iliyoko wilayani Bunda, akichangia hoja katika kikao cha Wadau wa pamba Mkoani humo kilichofanyika Mjini Bariadi lengo likiwa ni kujadili mstakabali wa zao hilo mkoani humo.
Mbunge wa Jimbo la Bariadi na Mmiliki wa Kiwanda cha pamba(Ginner), Mhe.Njalu Silanga akichangia hoja katika kikao cha Wadau wa  pamba Mkoani humo kilichofanyika Mjini Bariadi lengo likiwa ni kujadili mstakabali wa zao hilo mkoani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Mhe.Dkt. Joseph Chilongani akichangia hoja katika kikao cha Wadau wa pamba Mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi lengo likiwa ni kujadili mstakabali wa zao hilo mkoani humo.
Ndg.Sebastiani Max kutoka SHIRECU akichangia hoja katika kikao cha Wadau wa pamba Mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi lengo likiwa ni kujadili mstakabali wa zao la pamba mkoani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe.Tano Mwera akichangia hoja katika kikao cha Wadau wa pamba Mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi lengo likiwa ni kujadili mstakabali wa zao hilo mkoani humo.
Mkurugenzi Mtedaji wa Kampuni ya BioRe Tanzania inayojishughulisha na uzalishaji wa pamba hai(organic cotton)Ndg. Niranjan Pattni, akichangia hoja katika kikao cha Wadau wa pamba Mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi lengo likiwa ni kujadili mstakabali wa zao hilo mkoani humo.
Ndg. Stephen Lawrent (mwenye miwani) kutoka Kampuni ya inayojihusisha na Ununuzi wa Pamba ya Nyanza Cotton akichangia hoja katika kikao cha Wadau wa pamba Mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi lengo likiwa ni kujadili mstakabali wa zao hilo mkoani humo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Mhe.Lucas Hinda Mwaniyuki akichangia hoja katika kikao cha Wadau wa pamba Mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi lengo likiwa ni kujadili mstakabali wa zao hilo mkoani humo.
Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Martha Zongo akichangia hoja katika kikao cha Wadau wa pamba Mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi lengo likiwa ni kujadili mstakabali wa zao hilo mkoani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe.Benson Kilangi akichangia hoja katika kikao cha Wadau wa pamba Mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi lengo likiwa ni kujadili mstakabali wa zao hilo mkoani humo.
.Baadhi ya Wajumbe wa Kamti ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe.Dkt. Titus Kamani wakifuatilia hoja mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi ili kujadili suala la Kilimo cha Pamba mkoani hapo.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Maswa akichangia hoja katika kikao cha Wadau wa pamba Mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi lengo likiwa ni kujadili mstakabali wa zao hilo mkoani humo.
Ndg.Jeremia Malongo kutoka Kampuni ya VITRESS inayojishughulisha na ununuzi wa pamba Mkoani Simiyu akichangia hoja katika kikao cha Wadau wa pamba kilichofanyika Mjini Bariadi lengo likiwa ni kujadili mstakabali wa zao hilo mkoani humo.

No comments:

Post a Comment