Wednesday, September 6, 2017

RC MTAKA APEWA TUZO NA ASASI YA WAZALENDO NA MAENDELEO TANZANIA(AWAMATA)

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amepewa tuzo ya cheti na Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania(AWAMATA) ikiwa ni alama ya kutambua mchango wake na kazi  za kizalendo na maendeleo anazozifanya Mkoani humo.

Akikabidhi tuzo hiyo kwa niaba ya Mwenyekiti wa AWAMATA Taifa, Mwenyekiti wa AWAMATA Mkoa wa  Simiyu, Ndg. Joseph Gimonge Golyo amesema Asasi hiyo imehamasika kutoa tuzo ya cheti kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu kwa sababu ni mzalendo na amekuwa akifikiri juu ya maendeleo ya wananchi na namna mbalimbali za kuzalisha ajira kwa vijana.

Amesema Mhe.Mtaka ni moja ya viongozi wabunifu sana na kama kiongozi kijana amekuwa na maono makubwa yenye manufaa kwa wananchi wa Mkoa wa Simiyu na Taifa kwa ujumla, ambapo amehamasisha uanzishwaji wa viwanda katika Mkoa kupitia Kauli Mbiu ya “Wilaya Moja Bidhaa Moja Kiwanda Kimoja” na  Kilimo cha Umwagiliaji wilayani Busega.

“Mhe.Mtaka tumeanza kumfuatilia toka akiwa Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Wilaya ya Hai mpaka na baada ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, tumekaa kama asasi tukashawishika kumpa tuzo hii, kwa sababu amekuwa anafanya kazi ya kizalendo na maendeleo hasa anapoumiza kichwa kwa ajili ya kutengeneza ajira; tena kila wilaya kwenye mkoa wake ina kitu cha kufanya” alisema Golyo.

Akipokea tuzo hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ameishukuru Asasi ya AWAMATA kwa kutambua mchango wa viongozi wa Mkoa wa Simiyu na akabainisha kuwa imeipokea tuzo hiyo kwa niaba ya Viongozi wa Mkoa huo pamoja na wadau wote wanaounga mkono juhudi za Serikali katika maendeleo ya Mkoa na wananchi kwa ujumla.

Mtaka amesema viongozi wa mkoa huo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wataendelea kujenga nuru ya matumaini kwa vijana ambao matarajio yao makubwa ni kuona kuwa wanapata kitu cha kufanya ili waweze kuendesha maisha yao.

Ameongeza kuwa miradi mingi inayoendelea ya Kiwanda cha Chaki, kiwanda cha kusindika maziwa na mingine inayofanywa katika ngazi ya viwanda vidogo vidogo ilianzishwa kwa sababu, mkoa unataka kujenga utamaduni kwa wananchi hususani vijana kujua kwamba wanaweza kuthubutu kwa kuanzia ngazi ya chini.

“ Pale Mkula Busega tulianza na vijana waliokuwa wanatengeneza viatu pair mbili tumewapa mtaji wa milioni 12 wameongeza uzalishaji na tumeomba Baraza la uwezeshaji wananchi Kiuchumi watawapa fedha ili wanunue mashine kubwa, pia tunajipanga kwa kilimo cha umwagiliaji; tunataka kuwa Mkoa ambao wananchi wake wana kitu cha kufanya na wanakiona kwenye vitendo badala ya kukiona kwenye hotuba nzuri.”

Katika hatua nyingine Mtaka amewaambia viongozi wa AWAMATA kuwa, pamoja na kutoa tuzo kwa viogozi kama walivyofanya kwake wanapaswa pia kuwakosoa viongozi hususani vijana bila kuwaonea (kuwakosoa katika haki) pale wanapoona hawafanyi vizuri, hii itawasaidia kuthibitisha dhamira ya Mhe.Rais ya kuwateua, maana ya kupewa uongozi katika kipindi hiki na kubeba dhamana kwa vizazi vijavyo.

Wakati huo huo ametoa wito kwa Viongozi wenzake vijana kutimiza wajibu wao, kuepuka maneno yanayowasahaulisha walikotoka wanapozungumzia maisha ya vijana wenzao na kukubali kukosolewa, ili wajengwe kuwa viongozi wazuri wa leo na vizazi vijavyo; kwa kuwa matarajio ya Rais katika kuwateua ni kuwa na kizazi endelevu kwenye uongozi wa nchi.

Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania(AWAMATA) ni asasi ya Kiraia inayojishughulisha na uelimishaji wa uzalendo kwa Watanzania na kufundisha mbinu za kujitegemea ili kuondokana na umaskini pia inatoa tuzo kwa watu wanaofanya vizuri masuala mbalimbali ya kizalendo na kuwasaidia wananchi kutoka katika umaskini.  
Mwenyekiti wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania(AWAMATA) Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Ndg. Joseph Gimonge Golyo (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa huo Mhe.Anthony Mtaka, tuzo ya cheti kwa niaba ya Mwenyekiti wa UWAMATA Taifa, ambayo imetolewa kwa Mkuu huyu wa mkoa kama alama ya kutambua kazi  za kizalendo na maendeleo anazozifanya Mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akionesha tuzo ya cheti aliyokabidhiwa na Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania(AWAMATA) kama alama ya kutambua mchango wake na kazi  za kizalendo na maendeleo anazozifanya Mkoani humo.
Kutoka kulia Mwenyekiti wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania(AWAMATA) Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Ndg. Joseph Gimonge Golyo, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka, Katibu wa AMAWATA mkoa wa Dar es Salaam, Bibi. Millensasha Mneo na Afisa Uhusiano wa AWAMATA, Ndg Shushu Joel wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi tuzo ya cheti iliyotolewa kwa Mhe.Mtaka kama alama ya kutambua mchango wake na kazi  za kizalendo na maendeleo anazozifanya Mkoani humo
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu(wa tatu kulia) akiwa  katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa AWAMATA na wadau wengine wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya Mkuu  huyo wa Mkoa kukabidhiwa tuzo ya cheti na Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania(AWAMATA) kama alama ya kutambua kazi  za kizalendo na maendeleo anazozifanya Mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa waSimiyu, Mhe.Anthony Mtaka (kushoto) akipongezwa na Katibu wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania(AWAMATA)  Mkoa wa Dar es Salaam, Bibi. Millensasha Mneo mara baada ya kukabidhiwa tuzo ya cheti na Asasi hiyo ngazi ya Taifa  kama alama ya kutambua  mchango na kazi  za kizalendo na maendeleo anazozifanya Mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa waSimiyu, Mhe.Anthony Mtaka (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Afisa Vijana, Zena Mchujuko(kushoto) naAfisa Habari(kulia) wote watumishi katika Ofisi yake mara baada kukabidhiwa tuzo ya cheti na Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania(AWAMATA) kama alama ya kutambua mchango wake na kazi  za kizalendo na maendeleo anazozifanya Mkoani humo.
Mwenyekiti wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania(AWAMATA) Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Ndg. Joseph Gimonge Golyo akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu(hayupo pichani) kabla ya  kumkabidhi  tuzo ya cheti iliyotolewa na  Asasi hiyo Ngazi ya Taifa, kama alama ya kutambua mchango wake na  kazi  za kizalendo na maendeleo anazozifanya Mkoani humo
Katibu wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA)  Mkoa wa Dar es Salaam, Bibi. Millensasha Mneo akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu(hayupo pichani) kabla ya  kumkabidhi  tuzo ya cheti iliyotolewa na  Asasi hiyo Ngazi ya Taifa, kama alama ya kutambua mchango wake na kazi  za kizalendo na maendeleo anazozifanya Mkoani humo.

No comments:

Post a Comment