Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua jiko la kisasa linalo jengwa
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa na wanafunzi wa Mpwapwa sekondari
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa na Kamati ya ujenzi wa Mpwapwa sekondari
Baadhi ya madarasa ya Mpwapwa sekondari yaliyo karabatiwa
VIONGOZI wa Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma wameishukuru serikali kwa kukarabati sekondari ya Mpwapwa ambayo majengo yake yalikuwa yana hali mbaya.
Viongozi hao wametoa
shukrani hiyo mbele ya Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Mhe. Selemani Jafo
alipokuwa katika ziara ya kikazi kukagua ukarabati wa shule hiyo.
Shule hiyo ni miongoni mwa shule 88 kongwe zinazokarabatiwa na
serikali ambapo katika awamu ya kwanza ukarabati umeanza kwa shule 43.
Katika shule hiyo, Serikali imefanikiwa kujenga bweni moja jipya
la wasichana, ukarabati wa mabweni 12 ya wavulana, ukarabati wa vyumba vya
madarasa 22, bwalo la chakuka pamoja na jiko, maktaba, maabara tatu, ofisi za
walimu, mfumo wa maji na umeme ambapo jumla ya sh.bilioni 1.2 zimetumika.
Akizungumza na viongozi katika ziara yake,Naibu Waziri Jafo
ameipongeza Kamati ya ujenzi kwa kufanyakazi bila kuchoka na kufanikisha
kuibadili kabisa shule hiyo ambayo kwasasa imegeuka kuwa shule bora ya kisasa
tofauti na ilivyokuwa awali.
No comments:
Post a Comment