Sunday, September 10, 2017

DC MTATURU AFANYA KIKAO NA WADAU WA ELIMU WILAYA YA IKUNGI WAISHIO DAR ES SALAAM NA PWANI

Na Mathias Canal, Dar es salaam
 
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne  Mtaturu leo Septemba 10, 2017 amefanya kikao na wadau wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Ikungi waishio Jijini Dar es salaam na Mkoa wa Pwani ili kuwaeleza dhamira ya kuanzishwa kwake ikiwa ni pamoja na kukuza ufanisi na kiwango cha ufaulu katika Wilaya hiyo.

Katika kikao hicho wadau wamechangia jumla ya shilingi milioni 3,900,000 ikiwa ni ahadi, Mifuko 100 ya saruji na rasilimali hamasa kwa vijana wa waliohitimu masomo ya sayansi katika vyuo mbalimbali nchini watakaojitolea kufundisha katika shule zenye upungufu wa walimu sayansi katika Wilaya ya Ikungi.

Mhe Mtaturu amewaeleza washiriki wa kikao hicho namna ambavyo Uongozi wa Wilaya umejipanga kwa kuhusisha michango ya wadau na nguvu za wananchi kwa ujumla kwa kuchangia rasilimali fedha ama viwezeshi kama vile saruji, mchanga, kokoto na vitu vifaa vingine vya ujenzi.

Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika Lamada Hotel Jijini Dar es salaam akiwa ameambatana na Mwalimu Athumani Salum ambaye ni Afisa elimu Sekondari wa Wilaya ya Ikungi, Mhe Mtaturu alisema kuwa zipo changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu Wilayani Ikungi ikiwa ni pamoja na Upungufu wa nyumba za walimu, Vyumba vya madarasa, Ofisi za walimu, Maabara, Thamani mbalimbali, Matundu ya vyoo vya walimu na wanafunzi.

Mhe Mtaturu aliwaeleza wadau hao wa Mfuko wa elimu kuwa Wazo la kuanzisha Mfuko wa Elimu lilitokana na kikao cha wadau wa elimu alichokiitisha mwezi Disemba, 2016 na kubaini changamoto zinazoikabili sekta ya elimu ikiwemo kushuka kwa ufaulu wa wanafunzi kuanzia elimu ya msingi mpaka Sekondari.

Alisema Kikao hicho kuliadhimiwa maazimio 43 ambayo yalizaa wazo la kuanzisha mfuko wa elimu ambapo wazo hilo lilifikishwa kwenye baraza la madiwani na kupokelewa kwa kauli moja ndipo mwezi Aprili mwaka 2017 baraza liliridhia kuanzishwa mfuko na kuteua wajumbe 15 wa bodi ya mfuko wa elimu wa Wilaya ya Ikungi.

Mhe Mtaturu alisema kuwa ili kukabiliana na changamoto zote hizo Bodi ilibainisha kuhitajika jumla ya fedha taslimu shilingi bilioni 28.

Hata hivyo Baada ya vikao mbalimbali vya maamuzi Bodi ya mfuko wa elimu imebainisha  mpango mkakati wa miaka mitatu kwa mtazamo wa Shule zenye hali mbaya zaidi hivyo kuandaa makadirio ya gharama za shilingi Bilioni 3.

Mhe Mtaturu alisema kuwa ili kufanikisha mpango huu kwa wakati husika Bodi ilitoa mapendekezo ya wadau watakoombwa kuchangia mfuko ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi  kuchangia 3% ya mapato yake ya ndani.

Sambamba na hayo pia alielezea mikakati mbalimbali katika sekta ya kilimo ikiwa ni pamoja na kilimo ambapo alisema wananchi wengi wanafanya kilimo cha kujikimu badala ya kilimo cha biashara hivyo ili kukuza ufanisi wa pato la mkulima Uongozi wa Wilaya ya Ikungi umekusudia kutatoa miche ya mbegu za korosho 500,000 bure kwani ni zao rahisi kulima lisilohitaji uangalizi wa muda mrefu.

Alieza pia namna Wilaya hiyo ilivyojipanga katika sekta ya Afya, Miundombinu, Sekta ya Maji, na kuimarisha hali ya usalama ili wananchi kufanya kazi zao kwa ufasaha pasina wasiwasi wowote.

Kwa upande wa wadau wa elimu Wilaya ya Ikungi walimpongeza Mkuu huyo wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu kwa kuanzisha mfuko wa elimu wa Wilaya pamoja na kuwashirikisha namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali wilayani humo.

Wamemuhakikishia kuwa watatoa ushirikiano wa hali na mali ili kuinua sekta ya elimu na kuchagiza ufanisi wa kukuza maendeleo katika Wilaya hiyo na Taifa kwa ujumla wake.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne  Mtaturu akizungumza na wadau wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Ikungi waishio Jijini Dar es salaam na Mkoa wa Pwani Dhifa iliyofanyika leo Septemba 10, 2017katika Hoteli ya Lamada Jijini Dar es salaam
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne  Mtaturu akizungumza na wadau wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Ikungi waishio Jijini Dar es salaam na Mkoa wa Pwani Dhifa iliyofanyika leo Septemba 10, 2017katika Hoteli ya Lamada Jijini Dar es salaam
Mdau wa Mfuko wa elimu Wilaya ya Ikungi ambaye pia ni Afisa elimu Mkoa wa Dar es salam Mwalimu Khamis Lissu akichangia namna ya kuboresha elimu wilaya ya Ikungi mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa kikao na wadau wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Ikungi waishio Jijini Dar es salaam na Mkoa wa Pwani Dhifa iliyofanyika leo Septemba 10, 2017katika Hoteli ya Lamada Jijini Dar es salaam
Wadau wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Ikungi waishio Jijini Dar es salaam na Mkoa wa Pwani wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu katika Dhifa iliyofanyika leo Septemba 10, 2017katika Hoteli ya Lamada Jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisalimiana na Mzee Mjengi Gwau wakati wa kikao cha Wadau wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Ikungi waishio Jijini Dar es salaam na Mkoa wa Pwani katika, Dhifa iliyofanyika leo Septemba 10, 2017 katika Hoteli ya Lamada Jijini Dar es salaam.
Mdau wa Mfuko wa elimu Wilaya ya Ikungi Ndg Nkrumah Munjori akichangi  namna ya kuboresha elimu wilaya ya Ikungi mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa kikao na wadau wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Ikungi waishio Jijini Dar es salaam na Mkoa wa Pwani Dhifa iliyofanyika leo Septemba 10, 2017katika Hoteli ya Lamada Jijini Dar es salaam
Wadau wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Ikungi waishio Jijini Dar es salaam na Mkoa wa Pwani wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu katika Dhifa iliyofanyika leo Septemba 10, 2017katika Hoteli ya Lamada Jijini Dar es salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Ikungi Alhaji Salumu M. Chima Akielezea hatua zilizofikiwa na kamati ya Mfuko wa elimu Wilaya ya Ikungi na wadau wa mfuko huo waishio Dar es salaam
Mdau wa Mfuko wa elimu Wilaya ya Ikungi Mzee Mjengi Gwau akichangia namna ya kuboresha elimu wilaya ya Ikungi mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa kikao na wadau wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Ikungi waishio Jijini Dar es salaam na Mkoa wa Pwani Dhifa iliyofanyika leo Septemba 10, 2017katika Hoteli ya Lamada Jijini Dar es salaam
Mdau wa Mfuko wa elimu Wilaya ya Ikungi ambaye pia ni Afisa elimu Mkoa wa Dar es salam Mwalimu Khamis Lissu akifatilia kwa makini kikao na wadau wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Ikungi waishio Jijini Dar es salaam na Mkoa wa Pwani Dhifa iliyofanyika leo Septemba 10, 2017katika Hoteli ya Lamada Jijini Dar es salaam
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne  Mtaturu akizungumza na wadau wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Ikungi waishio Jijini Dar es salaam na Mkoa wa Pwani Dhifa iliyofanyika leo Septemba 10, 2017katika Hoteli ya Lamada Jijini Dar es salaam
Mdau wa Mfuko wa elimu Wilaya ya Ikungi Bi Khadija Kiimu akichangia namna ya kuboresha elimu wilaya ya Ikungi mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa kikao na wadau wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Ikungi waishio Jijini Dar es salaam na Mkoa wa Pwani Dhifa iliyofanyika leo Septemba 10, 2017katika Hoteli ya Lamada Jijini Dar es salaam
Mdau wa Mfuko wa elimu Wilaya ya Ikungi Ndg Omary Gwati akichangia namna ya kuboresha elimu wilaya ya Ikungi mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa kikao na wadau wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Ikungi waishio Jijini Dar es salaam na Mkoa wa Pwani Dhifa iliyofanyika leo Septemba 10, 2017katika Hoteli ya Lamada Jijini Dar es salaam
Mdau wa Mfuko wa elimu Wilaya ya Ikungi Ndg Josephat Bulali akichangia namna ya kuboresha elimu wilaya ya Ikungi mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa kikao na wadau wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Ikungi waishio Jijini Dar es salaam na Mkoa wa Pwani Dhifa iliyofanyika leo Septemba 10, 2017katika Hoteli ya Lamada Jijini Dar es salaam

No comments:

Post a Comment