Ujumbe kutoka Ofisi yaMakamu wa
Rais ukiongozwa na Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bi Ogenia Mpanduji
wakimsikiliza Mmiliki wa Mgodi wa Sambaru uliopo wilayani Ikungi Mkoani
Singida, Bwana Yusuf Mwandami walipofanya ziara ya kutembelea mgodi
huo.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya
Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais,Bi Magdalena Mtenga akiuliza swali kwa
mmiliki wa mgodi wa sambaru uliopo Ikungi Mkoani Singida mara baada ya
ujumbe toka Ofisi ya Makamu wa Rais kutembelea mgodi huo wa mwisho
katika picha ni Afisa madini kanda ya Singida aliyeongozana na ujumbe
huo Bi. Sofia Omary.
Mmiliki wa Mgodi mdogo wa dhahabu
wa Sambaru uliopo Ikungi Bwana Yusuf Mwandami akitoa maelekezo kwa
ujumbe huo juu ya mashine mbalimbalimbali zilizofungwa mgodini hapo
zitakavyokua zinafanya kazi. Wa kwanza kulia ni Afisa madini kanda ya
Singida aliyeongozana na ujumbe huo Bi. Sofia Omary.
Ujumbe kutoka Ofisi ya Makamu wa
rais ukiongozwa na Mkurugenzi wa sera na Mipango Bi Ogenia Mpanduji
pamoja na Mkurugenzi Msaidizi-Mazingira Bi. Magdalena Mtenga wakipata
maelezo juu ya uendeshaji wa mgodi mdogo wa dhahabu ulioko Ikungi Bwana
Ahmed Magoma
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya
Mazingira Bi Magdalena Mtenga (wa kwanza kulia) akimuuliza maswali
Mmiliki wa mgodi mdogo wa dhahabu ulioko Ikungi mkoani Singida Bwana
Ahmed Magoma wakati ya ziara ya Ujumbe toka Ofisi ya Makamu wa Rais
ilipotembelea mgodi huo.
No comments:
Post a Comment