Baada
ya onyesho la pili la Coke studio msimu wa tano kupitia luninga ya
Clouds kuacha gumzo kwa washabiki wengi wa muziki,mwishoni mwa wiki
katika onyesho la tatu walipagaishwa tena na kolabo za wasanii
mbalimbali zenye midundo ya kiafrika na zilizosukwa kwa ustadi mkubwa na
magwiji wa kutengeneza muziki .
Wasanii waliotoa burudani kwenye
onyesho la tatu ni mwanamuziki Nandy kutoka Tanzania ambaye amefanya
kolabo na mwanamuziki Betty G kutoka Ethiopia ambapo wameimba kwa pamoja
vibao vya Don’t break my heart na Mane Fistum, vilivyotengenezwa studio
kwa umahiri mkubwa na mtengenezaji wa muziki nguli nchini Nahreel.
Wasanii wengine ambao wamefanya
kolabo ya kuvutia katika onyesho hilo ni Khaligraph Jones kutoka nchini
Kenya akishirikiana na mwanamuziki Bruce Melodie kutoka nchini Rwanda.
Kwenye onyesho la pili, Ali Kiba
kutoka Tanzania, Patoranking kutoka Nigeria, Ozane kutoka Togo, Sami Dan
kutoka Ethiopia, Laura Beg kutoka Mauritus, Sauti Sol kutoka Kenya na
Chidinma kutoka Nigeria walionyesha umahiri wao katika tasnia ya muziki
na kutawala jukwaa katika onyesho lao lililotengenezwa na nguli wa
kutengeneza muziki wa studio barani Afrika kutoka nchini Nigeria,
MasterCraft.
Kupitia onyesho hili la Coke Studio linaloandaliwa na kampuni
ya Coca Cola muziki wa Tanzania unazidi kutangazwa ikiwemo vipaji vya
wanamuziki kutoka hapa nchini ambao wanashirikiana na wenzao kutoka
Afrika na linarushwa kwenye luninga kwenye nchi zaidi ya 50
Onyesho la Coca Studio msimu huu
barani Afrika linajumuisha wasanii kutoka katika nchi za Kenya, Uganda,
Tanzania, Rwanda, Ethiopia, Nigeria, Ghana, Angola, Zimbabwe, Afrika
Kusini, Togo, Cote d’Ivoire, Madagascar, Mauritius, Mozambique, DRC na
Cameroon.
Wasanii wa Tanzania waliopo katika
onyesho la Coke Studio msimu huu ni Ali Kiba, Rayvanny, Izzo Bizness,
na Nandy.Wengine kutoka nchi nyingine ni Khaligraph Jones na Band Becca
(Kenya),Sami Dan (Ethiopia),Bebe Cool, Eddy Kenzo, Sheebah, Ykee Benda (
Uganda).
Wengine ni Nasty C, Busiswa,
Mashayabhuqe kutoka Afrika ya Kusini, Youssoupha kutoka Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo, Runtown na Yemi kutoka Nigeria, Dji Tafinha
kutoka Angola, Laura Beg kutoka Mauritius,Jah Prayzah na Slapdee kutoka
Central Africa Republic, Bisa Kdei na Worlasi kutoka Ghana.
Tangia onyesho hili lianzishwe
limekuwa kiungo kikubwa cha kuwakutanisha wanamuziki wa Afrika kufanya
kazi kwa pamoja na kupiga muziki wenye vionjo kutoka sehemu mbalimbali
za Afrika ikiwemo kuleta burudani kubwa kwa washabiki wa muziki wa
kiafrika na kuwaunganisha waafrika hususani vijana kupitia muziki.
No comments:
Post a Comment