KAMATI
ya Utendaji ya Chama Cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania
(TASWA), iliyokutana Dar es Salaam jana Septemba 7, 2017, imepanga
Uchaguzi Mkuu wa chama hicho ufanyike Novemba 5, mwaka huu.
Uchaguzi
huo utafanyika Dar es Salaam katika ukumbi ambao utatangazwa na tayari
kamati imeaigiza sekreterieti ya TASWA, ifanye maandalizi kuhusu
uchaguzi huo, ikiwa ni pamoja na kulishirikisha Baraza la Michezo la
Taifa (BMT) kwa ajili ya usimamizi wa karibu.
Kikao
kimekubaliana watakaoshiriki uchaguzi huo ni wanachama wote wa TASWA
waliopo katika leja kuanzia Juni mwaka 2007 hadi Juni mwaka 2017,
wakiwemo walioingia uanachama wakati wa semina ya waandishi chipukizi
iliyofanyika Dar es Salaam Agosti mwaka 2015 na sharti kubwa ni kila
mwanachama kulipia ada ya mwaka mmoja.
Kwa
wanachama wengine wapya wanaotaka kujiunga, watafanya hivyo baada ya
uongozi mpya kuingia madarakani na kupewa utaratibu kulingana na Katiba
ya chama inavyoeleza na pia kwa kadri uongozi mpya utakaoingia
madarakani utakavyoona inafaa.
Kutokana
na hali hiyo wanachama wote wenye sifa hizo, wanatakiwa kulipia ada zao
kwa Mhazini Msaidizi, Zena Chande kuanzia leo hadi Septemba 30, mwaka
huu.
Uongozi
wa sasa wa TASWA uliingia madarakani mwaka 2014, ambapo Juma Pinto
alichaguliwa kuwa Mwenyekiti, Egbert Mkoko (Makamu Mwenyekiti), Amir
Mhando (Katibu Mkuu), Grace Hoka (Katibu Mkuu Msaidizi), Shija Richard
(Mhazini) na Zena Chande (Mhazini Msaidizi).
Wajumbe
ni Rehure Nyaulawa, Chacha Maginga, Mussa Juma, Mwani Nyangassa, Mroki
Mroki, Ibrahim Bakari na Majuto Omary anayeingia kwa nafasi yake ya
Mwenyekiti wa TASWA FC.
Ahsanteni,
Juma Pinto
Mwenyekiti TASWA
08/09/2017
No comments:
Post a Comment