Mkurugenzi wa Barabara toka
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi John Ngowi akielezea
jambo wakati wa kongamano la pili la majadiliano kuhusu uanzishwaji wa
Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT) leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka
kulia ni Mwenyekiti wa Kampuni ya EcomResearch ambayo ndio mshauri
mwelekezi wa uanzishwaji wa taasisi hiyo Profesa Godwin Mjema na
Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala toka wizara hiyo Bw. Stephen Mushi.
Mwenyekiti wa Kampuni ya
EcomResearch ambayo ndio mshauri mwelekezi wa uanzishwaji wa Taasisi ya
Teknolojia ya Ujenzi (ICoT), Profesa Godwin Mjema akifafanua jambo
wakati wa kongamano la pili la majadiliano kuhusu uanzishwaji wa taasisi
hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi wa Barabara toka
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi John Ngowi na
Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala toka wizara hiyo Bw. Stephen Mushi.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Bi. Segolena
Francis akifafanua jambo wakati wa kongamano la pili la majadiliano
kuhusu uanzishwaji wa Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT) leo Jijini
Dar es Salaam.
Mtaalamu wa Utafiti kutoka
Kampuni ya EcomResearch ambayo ndio mshauri mwelekezi wa uanzishwaji wa
Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT),akifafanua jambo wakati wa
kongamano la pili la majadiliano kuhusu uanzishwaji wa taasisi hiyo leo
Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa kongamano
la pili la majadiliano kuhusu uanzishwaji wa Taasisi ya Teknolojia ya
Ujenzi (ICoT) wakiwa katika kikundi cha majadiliano hayo yaliyofanyika
leo Jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo limewashirikisha wadau wa sekta
ya ujenzi kutoka sehemu mbalimbali.
Mkurugenzi wa Barabara toka
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi John Ngowi (wanne
kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa sekta ya ujenzi
mara baada ya kufungua kongamano la pili la majadiliano kuhusu
uanzishwaji wa Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT) leo Jijini Dar es
Salaam.
Picha na Idara ya Habari (MAELEZO)
………………………………………………………………………….
Serikali kupitia Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inatarajia kuanzisha Taasisi ya
Teknolojia ya Ujenzi (ICoT) ili kuweza kuzalisha wataalam wa ngazi ya
kati wenye ubobezi katika sekta ya ujenzi.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa
Barabara Mhandisi John Ngowi wakati wa kongamano la pili la kujadili
hatua mbalimbali zilizofikiwa juu ya uanzishwaji wa Taasisi hiyo leo
jijini Dar es Salaam.
Mhandisi Ngowi amesema kuwa
kuanzishwa kwa taasisi hiyo hapa nchini kutawezesha kuondoa pengo la
uwiano baina ya wahandisi na kada za chini kama mafundi sanifu na
mafundi mchundo ambao ndio wasimamizi wa karibu wakati kazi za ujenzi
zinapotekelezwa.
“Mpango mkakati wa Wizara yetu
pamoja na mambo mengine, unahusisha uimarishwaji wa sera zinazohusu
ujenzi kwa kujenga mazingira wezeshi,mafunzo ya ufundi na matumizi ya
teknolojia mkakati ambao utawezesha kutatua changamoto za umahiri na
ubobezi inayokabili sekta ya ujenzi,” amesisitiza Mhandisi Ngowi.
Aidha, Mhandisi Ngowi ameongeza
kuwa uanzishwaji wa taasisi hiyo itakuwa chachu ya kufikia azma ya
serikali ya awamu ya tano katika kuelekea uchumi wa kati wa viwanda
ifikapo mwaka 2025 kwa kuongeza rasilimali watu ambao ni muhimu katika
usanifu, usimamizi, ujenzi na ukarabati wa miundombinu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Kampuni ya EcomResearch ambayo ni mshauri wa uanzishwaji wa ICoT
Profesa Godwin Mjema amesema kuwa mipango ya uanzishwaji wake umefikia
hatua nzuri ambapo umeshirikisha wadau mbalimbali ili kujadili Kozi na
mitaala itakayotumika kufundishia.
“Sisi kazi yetu ni kushauri na
leo tumekutana na wadau kujadili hatua tuliyofikia, wadu watajadili na
kukubaliana na yale tuliyoandaa, wakikubaliana na sisi tutakabidhi kwa
wizara ambao ndio wamiliki na wao watawasilisha Baraza la Taifa Elimu ya
Ufundi (NACTE) kwa hatua za usajili,”. amesema Profesa Mjema.
Kuanzishwa kwa taasisi hii
kunatokana na kuendelea kupanuka kwa pengo kati ya waandisi na kada za
chini hali iliyotokana na vyuo vingi vya ufundi kupandishwa hadhi kuwa
vyuo vikuu katika miaka ya 1990 bila kuanzishwa vyuo vingine vya ngazi
ya kati hasa vya fani ya ujenzi.
No comments:
Post a Comment