Itachukua dakika 29 tu kutoka London hadi New-York.
Hivi karibuni watu wataweza kusafiri kutoka mji mmoja hadi mwingine
kutumia roketi, safari ambayo itachukua dakika chache tu, kulingana na
mjasiriamali Elon Musk.
Musk aliahidi haya katika kongamano moja nchini Australia.
Inasemekana kuwa itachukua dakika 29 tu kutoka London hadi New-York.
Musk amesema pia kuwa mwaka wa 2024, ataanza kuwasafirisha watu hadi
Mars. Kampuni yake ya SpaceX itaanza kujenga meli za kipekee
zitakazofanikisha haya, mwaka ujao.
Kwa sasa kampuni yake inatengeneza ain amoja tu ya roketi; aina ya BFR
ambayo inaweza kufanya kazi tofauti tofauti ikiwemo kupeleka watu kwenye
mwezi na Mars.
"Safari ambazo watu wengi wanaona kuwa ndefu zinaweza kukamilika kwa chini ya nusu-saa," aliambia umati wa watu mjini Adelaide.
"Baadhi ya wateja wetu wanataka kuona BFR ikiruka mara kadhaa kabla yaya kuwa na imani nayo," Musk alisema.
"Kwa hivyo tunachotaka kufanya ni kujenga roketi kadhaa aina ya Falcon 9
na Dragon, ili wateja wawe na urahisi, na ikiwa wanataka kutumia roketi
za kale, bado tuna kadhaa."
Musk, alianza mipango ya kufanikisha safari za Mars mwaka wa 2016, na amerejea na habari zaidi.
Musk amevutia watu wengi sana ambao wamependezwa na miradi yake. Na
ingawa ahadi zake mara nyingi zimechukua muda mrefu kutekeleza, baadhi
imetimia.
Hii ni pamoja na kutuma na kurejesha roketi 16 duniani baada ya roketi
hizo kumaliza misheni yao. Roketi mbili kati ya hizo 16 zimeweza
kusafiri tena mara ya pili.
Anasema cha muhimu sana kwake ni kuunda rtoiketi ambazo zinawza kutumika
tena na tena kama ndege, kwani ni inagharimu pesa nyingi sana
kutengeneza roketi.
No comments:
Post a Comment