Naibu waziri wa maji na Umwagiliaji Mhe Isack A. Kamwelwe (Mwenye suti nyeusi) akielekea kujionea Chanzo cha Mradi wa maji wa Kintinku/Lusilile katika Kijiji Cha Mbwasa Kata ya Makutupora, Tarafa ya Kintinku Wilayani Manyoni, kulia kwake ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu, Kushoto kwake ni Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki Mhe Daniel Mtuk.
Naibu waziri wa maji na Umwagiliaji Mhe Isack A. Kamwelwe alipotembelea Chanzo cha Mradi wa maji wa Kintinku/Lusilile katika Kijiji Cha Mbwasa Kata ya Makutupora, Tarafa ya Kintinku Wilayani Manyoni
Naibu waziri wa maji na Umwagiliaji Mhe Isack A. Kamwelwe akizungumza jambo mara baada ya kutembelea Chanzo cha Mradi wa maji wa Kintinku/Lusilile katika Kijiji Cha Mbwasa Kata ya Makutupora, Tarafa ya Kintinku Wilayani Manyoni
Naibu waziri wa maji na Umwagiliaji Mhe Isack A. Kamwelwe akikagua ujenzi wa eneo maalamu litakalotumika kwa ajili ya kuhifadhi umeme kwa ajili ya kusafirisha maji kuelekea katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Manyoni katika eneo la Mitoo.
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza jambo wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu waziri wa maji na Umwagiliaji Mhe Isack A. Kamwelwe kukagua utekelezaji wa ilani uchaguzi ya CCM 2015-2020
Naibu waziri wa maji na Umwagiliaji Mhe Isack A. Kamwelwe akisisitiza jambo mbele ya wananchi, Kulia kwake ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu
Naibu waziri wa maji na Umwagiliaji Mhe Isack A. Kamwelwe (Kulia) akisalimiana na wananchi wa Kitongoji cha Kaloleni mara baada ya kuwasili katika eneo hilo kujionea hali ya upatikanaji wa maji.
Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki Mhe Daniel Mtuka (Kulia) akizungumza jambo mbele ya Naibu waziri wa maji na Umwagiliaji Mhe Isack A. Kamwelwe (Kushoto) wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua miradi ya vyanzo vya maji.
Mfereji wa Skimu ya Umwagiliaji kijijini Itagata ukiwa katika hatua nzuri za ujenzi
Bwala la Skimu ya Umwagiliaji lililogomewa na wananchi wa kijiji cha Itagata mara baada ya kubaini kuwa linavuja kutokana na mashimo yaliyopo yanayopelekea upotevu wa maji.
Naibu waziri wa maji na Umwagiliaji Mhe Isack A.
Kamwelwe akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Itagata, Halmashauri ya Wilaya ya Itigi kuhusu namna bora ya kukamilisha Mradi wa Ujenzi wa Bwala la Skimu ya Umwagiliaji.
Kwa upande wake
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe
Miraji Jumanne Mtaturu ameielekeza Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya
kutoa taarifa ya utekelezaji wa upatikanaji wa maji kwenye kamati ya ulinzi na
usalama ili iwe rahisi kuwasilisha kwa wananchi waweze kutambua namna serikali
inavyotekeleza kwa vitendo uwezekano wa upatikanaji wa maji kirahisi.
Alisema kuwa
miongoni mwa changamoto kubwa inayowakabili wananchi Katika Wilaya hiyo na Taifa
kwa ujumla ni ugumu wa upatikanaji wa maji kwani kwani wanatumia umbali mrefu
kupata maji jambo ambalo linahatarisha maisha yao.
Mhe Mtaturu
alisema ili kukamilisha adhma ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli ambyo
imedhamiria kuboresha huduma mbalimbali ni lazima kujikita katika uboreshaji wa sekta ya maji na umwagiliaji,
afya, elimu pamoja na sekta zingine.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment