Mtendaji MKuu wa Uongozi
Institute Prof Joseph Semboja akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo
ya Uongozi kwa wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Manispaa,majiji na
Halmshauri leo Mjini Dodoma.
Picha zote na Daudi Manongi,MAELEZO,DODOMA.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe.
Josephine Matiro na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe.Richard Kasesela
wakimsikiliza Naibu Waziri-TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo (hayupo pichani)
wakati akifungua mafunzo ya siku tano kwa wakuu wa Wilaya na
Wakurugenzi wa Manispaa,Majiji na Halmshauri leo Mjini Dodoma.
Naibu Waziri-TAMISEMI
Mhe.Selemani Jafo akizungumza jambo na Naibu Katibu Mkuu-TAMISEMI
Mhe.Dkt Zainabu Chaula wakati wa mafunzo ya Uongozi kwa Wakuu wa Wilaya
na Wakurugenzi wa Manispaa,Majiji na Halmshauri yanayofanyika Mjini
Dodoma na kuendeshwa na Taasisi ya Uongozi.
Baadhi ya Wakurugenzi wa
Manispaa,Majiji na Halmshauri wanaohudhuria mafunzo ya Uongozi
yanayoendeshwa na Taasisi ya Uongozi wakisikiliza mada mbalimbali
katika mafunzo hayo leo Mjini Dodoma.
Naibu Waziri-TAMISEMI
Mhe.Selemani Jafo akizungumza na Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa
Manispaa,Majiji na Halmshauri wakati akifungua mafunzo ya siku tano
yanayoendeshwa na Taasisi ya Uongozi leo Mjini Dodoma.
Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni Ally Happi akitoa neon la shukrani kwa mgeni
rasmi wakati wa mafunzo ya uongozi yanayoendeshwa na Ofisi ya Rais
Tamisemi kwa ushirikiano na Taasisi ya Uongozi
…………………………………………………………………………………
Nteghenjwa Hosseah, Tamisemi – Dodoma.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo
amewataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wote nchini kutekeleza
majukumu yao kwa ufanisi ili kutimiza matarajio ya watanzania ambao
wanaitegemea Wizara hii kama chachu ya mabadiliko katika utendaji kazi
wa Serikali ya awamu ya Tano.
Mhe.Jafo ameyasema hayo wakati wa
ufunguzi wa mafunzo kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri
za Mikoa ya Dar es Salaam, Shinyanga, Mbeya, Songwe, Rukwa, Ruvuma,
Iringa na Njombe yanayoendeshwa na Ofisi ya Rais Tamisemi kwa
ushirikiano na Taasisi ya Uongozi.
Akiungumza katika ufunguzi wa
mafunzo hayo Mhe.Jafo amewataka viongozi hao kutumikia Wananchi kwa
kuzingatia Taratibu, Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma huku
wakizingatia mipaka yao ya Utawala, kuboresha mahusiano katika maeneo ya
kazi na kuhakikisha hakuna muingiliano wa majukumu baina ya viongozi
wa Wilaya na Halmashauri.
“Nafahamu baadhi viongozi
mlitokea katika sekta binafsi na humkuwa mnafahamu vizuri utendaji kazi
wa shughuli za Serikali hata hivyo mmefanikiwa kwa kipindi chote
kutenda kwa kadiri ya maelekezo ya Serikali,vipaumbele na miongozo
mbalimbali iliyotolewa pia mmejitahidi kutoa huduma bora ukiachilia
mbali mapungufu madogo madogo ambayo tumeyabaina na kuyashuhudia katika
baadhi ya maeneo” alisema Jafo.
Aliongeza kuwa “kupitia mafunzo
haya ni imani yangu kuwa wote sasa tutakuwa na uelewa wa pamoja wa
kufanya kazi Kimkakati ili kuwaletea wananchi maendeleo huku mkifahamu
vyema Muundo wa Serikali na namna inavyofanya kazi kwa kuzingatia mipaka
na mgawanyo wa majukumu, Itifaki, utunzaji wa Siri za Serikali na
maadili ya viongozi wa Umma”.
Aidha Mhe. Jafo aliwataka
viongozi hao kuendelea kusimamia nidhamu ya watumishi, kuendeleza
mapambano dhidi ya Dawa la kulevya, kulinda amani na utulivu katika
maeneo yao huku wakisimamia kwa makini mapato na matumizi ya Fedha za
Serikali na kusisitiza matumizi ya mifumo ya Kielektroniki katika
ukusanyaji wa mapato ya Serikali.
Akimkaribisha Mgeni rasmi katika
mafunzo hayo Naibu Katibu Tamisemi anayeshughulikia Afya Dkt. Zainabu
Chaula amesema kitu cha msingi kati yetu sisi watendaji ni umoja ambao
kupitia huo utatuleta Ushindi na muongozo wa utendaji wetu uko kwenye
ilani ya Chama cha Mapindui hivyo kila mmoja wetu arejee Ilani ile ili
afahamu nini anachotakiwa kukifanya katika kipindi hiki cha miaka
mitano.
Awali akitoa taarifa ya
utangulizi kwa mgeni rasmi na washiriki wa mafunzo hayo Mtendaji Mkuu wa
Taasisi ya Uongozi Prof. Joseph Semboja alisema mafunzo haya
yanatolewa na wataalamu walioboea katika masuala ya uongozi na
yatafanyika kwa muda wa siku tano kwa viongozi aidi ya 72.
Aliongeza kuwa maeneo ambayo
yatajengewa uwezo ni namna bora ya kufanya maamuzi ya kimkakati
yanayozingatia mahitaji na manufaa mapana ya Taifa, namna bora ya
kuongoza watu na kusimamia Rasilimali za Taifa na pia jinsi ya
kujijengea Sifa za kiungozi ambazo zinaleta heshima kwa jamii,
kuaminika na kutegemwa katika kuleta mabadiliko.
Mafunzo haya yamepangwa kufanyika
katika awamu nne(4) ambapo awamu mbili tayari zimekwsihafanyika
ziliojumuisha Wah. Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kutoka Mikoa kumi na
mbili(12) ya Dodoma, Morogoro, Singida, Tabora, Kigoma, Katavi, Kagera,
Mwana, Mara, Simiyu, Geita na Manyara.
Awamu ya kwanzaya mafunzo haya ya
Uongozi yalifanyika Mwezi Mei, 2017 na yalifunguliwa na Waziri Mkuu
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa na
awamu ya mwisho inatarajiwa kufanyika kabla ya mwezi Disemba 2017.
No comments:
Post a Comment