Naibu Waziri wa nchi, Ofisi ya
Rais, Tamisemi Selemani Jafo akizindua rasmi Maadhimisho ya siku ya
wazee yaliyozinduliwa kitaifa katika viwanja cha Nyerere Square Mkoani
Dodoma.
Baadhi ya wazee waliohudhuria katika uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya wazee Duniani.
Mmoja wa wazee Mzee Kachenje akitoa neno la shukrani katika uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya wazee Duniani.
……………..
Naibu Waziri wa nchi, Ofisi ya
Rais, Tamisemi Selemani Jafo ametoa maagizo kwa ngapi za mikoa na wilaya
kusimama imara katika kuwalinde wazee dhidi ya mauaji ya kikatili
yanayofanywa na watu wasio na roho za ubinadamu.
Jafo aliyasema hayo leo alipokuwa
akizindua rasmi Maadhimisho ya siku ya wazee yaliyozinduliwa kitaifa
katika viwanja cha Nyerere Square Mkoani Dodoma.
Amesema serikali inasikitishwa na
Mauaji wa wazee ambayo yamekuwa yakiendelea hususan katika mikoa ya
kanda ya ziwa kitendo kinacho ashiria unyama uliopitiliza.
Jafo amekemea tabia hiyo mbaya ambayo inaharibu sifa ya nchi na utamaduni.
Kutokana na hali hiyo, Jafo
amewataka wakuu wa mikoa na wilaya kupitia kamati zao za ulinzi na
usalama kuwachukulia hatua kali watu wote wanaoendesha vitendo hivyo
viovu hapa nchini.
Maadhimisho hayo yamezinduliwa
rasmi Leo kitaifa ambapo wazee mbalimbali wamepata fursa ya kupimwa afya
zao bure katika viwanja hivyo na kilele chake cha kitafanyika Oktoba
mosi, mwaka huu.
No comments:
Post a Comment