Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo
akizungumza katika uwekaji jiwe la msingi kwenye ujenzi wa jengo la Halmashauri
ya wilaya ya Gairo mkoani Morogoro.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akiweka jiwe la msingi katika jengo la Halmashauri ya wilaya ya Gairo mkoani Morogoro.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo akimsikiliza Mkandarasi wa Wakala wa Barabara akitoa taarifa ya ujenzi wa barabara za Gairo mjini.
Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Gairo mkoani Morogoro wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akiweka jiwe la msingi katika jengo la Halmashauri ya wilaya ya Gairo mkoani Morogoro.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo akimsikiliza Mkandarasi wa Wakala wa Barabara akitoa taarifa ya ujenzi wa barabara za Gairo mjini.
Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Gairo mkoani Morogoro wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tamisemi Mhe. Selemani Jafo
amewapongeza halmashauri ya wilaya ya Gairo mkoani Morogoro kwa
kutekeleza maagizo ya serikali kwa maendeleo mazuri ya ujenzi wa majengo ya
Ofisi ya halmashauri hiyo.
Jafo Ametoa pongezi hizo Leo alipokuwa akiweka jiwe la msingi la
jengo hilo la kisasa ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 75.
Ujenzi huo umetokana na agizo alilolitoa Agosti 17, mwaka huu, alipotembelea
jengo la la halmashauri ya Chamwino mkoani Dodoma na kuagiza halmashauri yeyote
ambaye imepewa fedha za ujenzi wa Ofisi lakini zitakuwa hazijaanza ujenzi baada
ya mwezi mmoja baada ya tarehe hiyo zingenyang'anywa fedha hizo na kupelekwa
katika halmashauri ambazo wanaendele na ujenzi.
Akizungumza katika uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la Halmashauri
ya Gairo iliyopo mkoani Morogoro, Jafo amesema halmashauri hiyo imekuwa ya mfano
kwa kutekeleza maagizo yake.
Amesema halmashauri hiyo imeamua kujichimbia kwenye ujenzi huo
kwa kutumia mkandarasi Pacha Construction Company ambaye amefanya kazi kubwa na
nzuri ndani ya muda mfupi.
Hata hivyo, Naibu Waziri Jafo amewaagiza makatibu Tawala wa
mikoa yote ambayo halmashauri zao zilipatiwa fedha lakini bado hawajaanza
ujenzi mpaka sasa wawasilishe majina ya halmashauri hizo kabla ya Oktoba 10,
mwaka huu ili mchakato wa kuzihamisha fedha hizo ufanyike mara moja kwa
kuzipeleka fedha hizo katika halmashauri zinazo endelea na ujenzi kwasasa.
Jafo anaendelea na ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo
katika mikoa mbalimbali hapa nchini kwa lengo la kubaini hatua za utekelezaji
wa miradi hiyo na kupima kama miradi hiyo inazingatia thamani ya fedha.
Katika hatua nyingine, Jafo amekagua ujenzi wa barabara za Gairo
mjini huku akimhimiza meneja wa wakala wa barabara vijijini(Tarura) kuhakikisha
anasimamia ujenzi huo ili ifikapo mwaka 2019 ahadi zote alizozitoa Rais Dk.John
Magufuli katika barabara za halmashauri hiyo ziwe kukamilika.
Barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 3.5 inajengwa na
mkandarasi C.G.I contractors LTD.
Akikagua barabara hiyo amewahakikishia wananchi kuwa serikali
itafanya jitihada katika kuhakikisha barabara zinajengwa na kwa kiwango kinachotakiwa
na kutoa fedha kwa wakati ili mkandarasi aliyepo aweze kumaliza kazi kama
ilivyopangwa.
Awali akitoa taarifa ya ujenzi wa barabara hiyo mkandarasi
Stephen Aloyce amesema ujenzi wa barabara hiyo umekamilika kwa asilimia 70 na
kuiomba serikali kukamilisha malipo ya shilingi Bilioni 1.5 ili kumalizia kazi
iliyobaki kabla ya kipindi cha mvua kuanza.
Awali akizungumza na watumishi kabla ya kukagua barabara hiyo,
Jafo amesema kutokana na taarifa ya ukaguzi iliyotolewa halmashauri hiyo ni
moja ya halmashauri 6 zilizofanya vibaya katika mfuko wa barabara jambo ambalo
linapaswa kusimamiwa vizuri kwa sasa ili lisijirudie tena.
"Taarifa ya ukaguzi inaonyesha Gairo ni moja ya halmashauri
6 zinazofanya vibaya,hili hatutalivumilia,taarifa hiyo ipo nitaiangalia na kama
kuna mtu alishiriki katika hilo hata kama hayupo hapa tutamchukulia
hatua,"amesisitiza Jafo.
Amewataka kuwa makini na ubora wa barabara zinazojengwa
kulingana na thamani halisi ya miradi hiyo ili barabara zinazojengwa zisije
kuharibika baada ya muda mfupi.
Naye, Mbunge wa jimbo la Gairo Ahmed Shabiby
ameishukuru serikali kwa jitihada zake za kutatua kero mbalimbali
zinazowakabili wananchi huku akiiomba serikali kuwasaidia kutatua kero ya maji ambayo
bado inawaumiza wananchi hao.
No comments:
Post a Comment