Mbunge wa Jimbo La Singida Magharibi Mhe Elibariki Kingu akizungumza
na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya
ya Ikungi ulioketi kuchagua viongozi wapya watakaoiongoza jumuiya hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne
Mtaturu (Mwenye shati la Njano), Mbunge wa Jimbo la
Singida Mgharibi Mhe Elibariki Kingu (Wa Kwanza kushoto Pichani) na
viongozi wengine wakifatilia Mkutano Mkuu wa Umoja wa
Vijana Wilaya ya Ikungi katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Ikungi.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne
Mtaturu ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya Siasa Wilaya akizungumza
na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya
ya Ikungi ulioketi kuchagua uongozi wapya watakaoiongoza jumuiya hiyo.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya
ya Ikungi wakimsikiliza mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano huo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne
Mtaturu kabla ya kuchagua uongozi wapya kuongoza jumuiya hiyo ngazi ya Wilaya.
Na
Mathias Canal, Singida
Mbunge wa Jimbo la
Singida Magharibi Mhe Elibariki Kingu ametajwa kama Kiongozi makini anayejali
maslahi ya wananchi wa Jimbo, Wilaya, Mkoa na Taifa kwa ujumla katika kipindi
kifupi cha utendaji wake tangu alipochaguliwa na wananchi Octoba 25, 2015.
Heko hiyo imetolewa na Mkuu
wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati akizungumza na wajumbe wa
Mkutano Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Ikungi
kwenye mkutano ambao ajenda yake kubwa ni uchaguzi wa uongozi wa jumuiya hiyo
ngazi ya Wilaya.
Mbele ya wajumbe hao
katika Mkutano ulifanyika kwenye ukumbi wa shule ya Sekondari Ikungi Mhe
Mtaturu alisema kuwa Mbunge huyo amekuwa mfano wa kuigwa kwani amejikita katika
shughuli za maendeleo zaidi katika jimbo lake jambo ambalo linaamsha ari kwa
wananchi kushiriki shughuli za maendeleo.
Aliwasihi wananchi kwa
ujumla kuendelea kumuunga mkono mbunge huyo kwa ushirikiano wake na viongozi wa
serikali za mitaa na Madiwani wa Kata zote sambamba na kumuunga mkoano
mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kwa weledi na ufanisi wanaoufanya
katika uwajibikaji.
Mhe Mtaturu alisema
kuwa Jimbo la Singida Magharibi ndilo pekee katika Wilaya ya Ikungi ambalo
limeonekana kuwa katika ramani ya uwajibikaji kupitia mbunge wake tofauti
kabisa na Jimbo la Singida Mashariki ambalo maendeleo yake yanasuasua kutokana
na chuki za kisiasa.
Aliongeza kuwa Mbunge
Kingu amekuwa ni kinara wa kusemea hoja na changamoto za wananchi wa Wilaya ya
Ikungi kwa ujumla mara kwa mara katika kipindi chote anapokuwa Bungeni nanje ya
Bunge nakuongeza kuwa huo ndio uwakilishi unaotakiwa.
Akizungumza kabla ya
kuanza kwa uchaguzi wa viongozi wa jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi CCM
Wilaya ya Ikungi Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Mhe Elibariki Kingu
alisema kuwa kwa sasa Wilaya ya Ikungi imepata kiongozi imara ambaye anajali
maslahi ya wananchi hivyo imani yake maendeleo yatazidi kuimarika kwa wananchi.
Aliwasihi Vijana
kushikamana na kuchagua kiongozi bora na si bora kiongozi ili kuendeleza
ufanisi wa jumuiya hiyo ambayo ndio muhimili wa Cham Cha Mapinduzi.
Aidha, alisema
ataendeleza zaidi ushirikiano baina yake ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji
Jumanne Mtaturu ili kuwanufaisha wananchi na kuboresha zaidi umoja na
mshikamano uliopo pasina kuwabagua wananchi kwa itikadi za Chama, Dini ama Kabila.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment