Kikosi cha Yanga
kimepanga kwenda kuweka kambi ya pamoja Pemba, Zanzibar kujiandaa na
mechi ya Ngao ya Jamii watakayocheza dhidi ya watani wao wa jadi Simba.
Mechi hiyo inatarajiwa kupigwa Agosti 23, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kambi hiyo itakuwa ya
pili kwa Yanga kutoka nje ya Jiji la Dar es Salaam baada ya hivi
karibuni kurejea kutokea Bigwa mkoani Morogoro ambako walikaa kwa wiki
mbili.
Katibu Mkuu wa Yanga,
Boniface Mkwasa alisema wameichagua Pemba kutokana na utulivu ili Kocha
Mkuu Mzambia, George Lwandamina apate nafasi ya kukiandaa kikosi hicho
vizuri.
Mkwasa alisema, timu hiyo itarejea jijini Dar siku moja kabla ya mechi hiyo ya Ngao ya Jamii.
Aliongeza kuwa,
maandalizi ya kambi hiyo tayari yamekamilika na wametuma watu kwa ajili
ya kuandaa kambi hiyo itakayofikia timu yao.
“Tutaondoka Dar
Jumapili asubuhi kuelekea Unguja, hapo tutacheza mechi ya kirafiki dhidi
ya Mlandege, usiku wa siku hiyohiyo, baada ya hapo Jumatatu tutaondoka
kwenda Pemba,” alisema Mkwasa.
No comments:
Post a Comment