Thursday, August 10, 2017

KATIBU MTENDAJI BODI YA FILAMU AFUNGA SEMINA YA MAMENEJA WA USAMBAZAJI WA KAZI ZA FILAMU KUTOKA MIKOA 25 YA TANZANIA

Pix 1
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi  Mkuu wa Barazani Entertainment Bw. John Kalage (Kulia) alipotembelea ofisi hizo leo Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufunga semina ya mameneja wa usambazaji wa kazi za filamu kutoka mikoa 25 ya Tanzania.
Pix 2
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo (kushoto) akiteta jambo na viongozi wa Barazani Entertainment kabla ya kufunga semina ya mameneja wa usambazaji wa kazi za filamu kutoka mikoa 25 ya Tanzania leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni mkuu wa Mawasiliano kutoka Barazani Entertainment Bw. Jacob Steven na katikati ni Mkurugenzi  Mkuu wa Barazani Entertainment Bw. John Kalage
Pix 3
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo (katikati) akizungumza na mameneja wa usambazaji wa kazi za filamu (hawapo pichani) kabla ya kufunga semina elekezi kwa mameneja hao leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Barazani Entertainment Bw. John Kalage na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha uenezi Bw. Singo Mtambalike
Pix 4
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo (katikati) katika picha ya pamoja na viongozi wa Barazani Entertainment na mameneja wa usambazaji kazi za filamu baada ya kufunga semina elekezi kwa mameneja hao leo Jijini Dar es Salaam.
Picha na: Genofeva Matemu – WHUSM

No comments:

Post a Comment