Sunday, August 20, 2017

Wazo Huru Blog yatambulishwa rasmi Wilayani IKUNGI...!

Mkuu wa wilaya ya Ikungi, Mhe Miraji Mtaturu (kushoto), akimkabidhi CD Mwenyekiti wa mtandao wa Wazo Huru Blog Ndg Mathias Canal kwenye uzinduzi wa albamu ya mwimbaji Elineema Babu

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu amenipa wasaa wa kuwasalimu wananchi wa Ikungi walizuru katika Uzinduzi wa Albamu ya Mwimbaji Elineema Babu ambapo alianza kuutambulisha Mtandao wa Wazo Huru Blog kwa kazi kubwa tunayoifanya ya kuhabarisha Umma wa Watanzania kuhusu maendeleo Yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli ambapo kwa kauli moja Mtandao Wetu pamoja na kazi ya kutoa taarifa Mbalimbali kwa Wananchi pia tunaunga mkono jukumu kubwa linalofanywa na Rais katika kuinua uchumu wa Watanzania.

Pamoja na kuitwa Jukwaani kwa kushtukizwa lakini nimeunga mkono kazi ya Mwimbaji Elineema Babu kwa kuchangia shilingi 100,000 huku Mkuu wa Wilaya akichangia shilingi shilingi Mil 1 ambapo jumla ya fedha zote zilizokusanywa ilikuwa Ni shilingi Milioni 3.1 

Wakati Mwema...!
Mathias Canal
Mwenyekiti Wazo Huru Blog
0756413465
Ikungi-Singida

No comments:

Post a Comment