Friday, August 11, 2017

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU TANZANIA (TFS) WATII AGIZO LA RAIS MAGUFULI LA KUANZA KUKUSANYA MADUHULI KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI

MBAO (2)
Baadhi ya mazao ya Misitu zikiwemo mbao  ambazo zitakuwa zikukusanywa kwa njia ya kielektroni kupitia  mfumo wa ukusanyaji maduhuli uliosanifiwa na Wizara ya Fedha na Mipango unaoitwa Government Electronic Payment Gateaway-GEPG ikiwa ni kutii agizo la Serikali ya awamu ya tano ya  Rais John Magufuli  ya kuzitaka Taasisi za serikali kujiunga na mfumo huo. 
Picha na Lusungu Helela
……………………….
Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) imeanza utekelezaji wa ukusanyaji wa maduhuli kwa njia ya kielektroniki kufuatia marekebisho ya sheria ya fedha ya mwaka 2017 na maelekezo ya serikali ya awamu ya tano ambao umezitaka Taasisi za serikali kujiunga na mfumo wa ukusanyaji maduhuli uliosanifiwa na Wizara ya Fedha na Mipango unaoitwa Government electronic Payment Gateaway-GEPG.   

Akitoa ufafanuzi huo jana jijini Dar es Salaam, Mhasibu Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Peter Mwakosya amesema mashamba yote na ofisi za mameneja (DFM’s) wa Taasisi hiyo zimeunganishwa katika mfumo huo.      

Aidha amesema kutokana na mazingira ya vizuia(Checkpoints)  kutokidhi mahitaji ya mfumo huo na hasa kushindwa kuhifadhi vitendea kazi kama kompyuta na printa kwa sasa wakala inaendelea kuunganisha kwenye mfumo vizuia vyote kwa kutumia vifaa maalum (Point of sales-POS). 

Amebainisha kwamba vifaa hivyo vitatumika kukusanya maduhuli na kuhakiki uhalali wa nyaraka zinazokaguliwa katika vituo vyote vya ukaguzi wa mazao ya misitu na nyuki kwa kipindi hiki ambacho  vinaendelea kuunganishwa vizuia kwenye mfumo wa moja kwa moja.           
        
 Mwakosya amesisitiza maduhuli yote yatakayokusanywa kwenye vizuia yanawasilishwa Ofisi za mameneja wa Misitu wa wilaya mapema ili yaingizwe kwenye mfumo.

 Pia amewakumbusha wateja wote wa Mazao ya Misitu na nyuki kuzingatia kwamba wanatakiwa kupata hati za madai (Bill) katika mfumo kabla ya kwenda kufanya Malipo.                     

Aidha, amewakumbusha wateja wa bidhaa za Misitu na nyuki kwamba stakabadhi zilizokuwa zikitumika kabla ya mfumo huo (ERV) hazitaendelea kutumika katika vituo vilivyounganishwa na mfumo.

No comments:

Post a Comment