Mkuu
wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda, akizungumza wakati akifungua mafunzo
ya siku moja kwa maofisa ugani wa wilaya hiyo mjini hapa leo. Mafunzo
hayo yameandaliwa
na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kupitia Jukwaa la
Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB). Kutoka kushoto ni Ofisa
Kilimo na Umwagiliaji wa Wilaya ya Mtwara, Joseph Tesha, Kaimu Katibu
Tawala, Francis Mkuti na Mshauri wa Kilimo Mkoa wa Mtwara, Ally
Linjenje.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Mtwara, George Mrisho, akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Maofisa Ugani wakijitambulisha kwa mkuu wa wilaya hiyo ambaye alikuwa mgeni rasmi.
Mkutano na maofisa ugani ukiendelea.
Mafunzo yakitolewa.
Mwezeshaji kutoka OFAB, Dk. Emmarold Mneney, akitoa mada kuhusu matumizi ya bioteknolojia na sayansi katika kilimo.
Ofisa Kilimo Mohamed Kaid kutoka wilaya hiyo, akichangia jambo.
Ofisa Kilimo kutoka Kata ya Msanga Mkuu, Maonyesho Bakari Said, akichangia katika mafunzo hayo.
Ofisa Kilimo Hamidu Ndago kutoka wilaya hiyo, akichangia jambo.
Ofisa Kilimo na Umwagiliaji wa Wilaya ya Mtwara, Joseph Tesha, akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Mtafiti
wa Mazao ya Mizizi kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo, Naliendele
Mtwara, Benadetha Kimata, akitoa mada kuhusu kilimo bora cha mhogo.
Wawezeshaji
wa mafunzo ya kutumia teknolojia katika kilimo kutoka COSTECH wakiwa
kikazi zaidi katika mafunzo hayo. Kutoka kulia ni Mtafiti, Dk.Nicholaus
Nyange, Rose Soloka na Bestina Daniel.
Na Dotto Mwaibale, Mtwara
MKUU wa
Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda amesema vipindi vya kilimo katika vyombo
vya habari vitasaidia kuinua sekta ya kilimo nchini.
Mmanda
ameyasema hayo mjini hapa leo wakati akifungua mafunzo ya namna ya
kutumia sayansi na teknolojia katika kuboresha kilimo kwa maofisa ugani
kutoka Halmashauri ya wilaya ya Mtwara na Halmashauri ya Manispaa ya
Mtwara ambayo yameandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia
(COSTECH) kupitia Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo
(OFAB).
” Nitoe
mwito kwa wizara ya kilimo, mifugo na uvuvi pamoja na Costech kuandaa
vipindi kwa njia ya radio na televisheni na machapisho mbalimbali kama
magazeti ili kuhamasisha kilimo bora jambo litakalosaidia kuinua sekta
ya kilimo hapa nchini na vijana wataweza kujifunza kuhusu kilimo badala
ya kuangalia vipindi vya visivyo na tija hasa katika wakati huu wa nchi
yetu kuelekea katika uchumi wa viwanda” alisema Mmanda.
Katika
hatua nyingine Mmanda amewataka maofisa ugani katika wilayani wajenge
mazoea ya kwenda kushinda na wakulima mashambani ili waweze kutoa
utaalamu ambao utawezesha kupatikana kwa mazao mengi na bora.
Alisema
haiwezekani mkulima kupata mazao bora bila kupatiwa ushauri na ofisa
ugani na hivyo akasisitiza kuwa watalamu hao waache tabia ya kukaa
maofisini, badala yake wakafanye kazi waliyoajiriwa ambayo ni kutoa
ushauri kwa wakulima.
Mmanda
alisema kilimo ni sayansi, hivyo kuna haja ya wagavi kupatiwa mafuzo ya
mara kwa mara kutoka kwa watafiti ambao wamekuwa wanafanya tafiti
mbalimbali za namna ya kuboresha kilimo huku akisisitiza ushirikiano
kati ya mkulima, ofisa ugani na mtafiti kuwa ni muhimu.
Mwezeshaji
kutoka OFAB, Dk. Emmarold Mneney aliwaambia maofisa ugani hao kuwa
wameamua kutoa mafuzo hayo kwa kuwa wanaamini kwamba changamoto
zinazokabili kilimo ni nyingi hasa magonjwa ya mazao, wadudu waharibifu
pamoja na kukosekana kwa mvua za kutosha.
Alisisitiza
kuwa mkulima ili aweze kuwa na kilimo chenye tija, lazima uongezee
udongo wako lishe, utibie mimea yako kama wewe unavyotibiwa na dawa ili
yapone na yatoe mazao mengi. Alisema sayansi ipo kwa ajili ya kumfanya
mkulima apate mazao mengine na sio kuendelea kuwa maskini kama ilivyo
sasa.
“Tuko
hapa kuelezea namna teknolojia hizi ambazo zinasaidia kukabiliana na
changamoto hizo, lengo ni kutaka wakulima wetu wazalishe kwa tija nchi
ijitosheleze kwa chakula lakini pia mkulima auze mazao yake na kupata
faida,” alisema Dk. Mneney.
No comments:
Post a Comment