Saturday, August 12, 2017

Trump ampongeza Vladimir Putin kwa kuwafukuza wanadiplomasia wa Marekani

media
Rais wa Marekani Donald Trump amesema anapongza uamuzi wa Vladimir Putin kuisaidia Marekani kuokoa fedha ilizokua ikitumia kwa afisi zake nchini Urusi.

Rais wa Marekani Donald Trump amepongeza uamuzi wa Rais wa Urusi Vladimir Putin wa kuwafukuza wafanyakazi 755 wa afisi za balozi za Marekani nchini Urusi.

Hivi karibuni Rais Putin aaliagiza kuondoka wafanyakazi 755 kutoka afisi za kibalozi za Marekani nchini Urusi, akilipiza kisasi hatua ya Marekani kuiwekea Urisi vikwazo zaidi.

Bw Putin alisema wafanyakazi wao walitakiwa kuondoka kufikia tarehe 1 Septemba, na kufikisha idadi ya wafanyakazi katika afisi za kibalozi wa Marekani hadi 455, sawa na wafanyakazi wa kibalozi wa Urusi walio Washington.

Katika mkutano na waandishi wa habari mjini New Jersey, Rais Donal Trump amesema anapongza uamuzi wa Vladimir Putin kuisaidia Marekani kuokoa fedha ilizokua ikitumia kwa afisi zake nchini Urusi.

Hata hivyo uchunguzi unaendelea nchini Marekani kuhusu madai ya Urusi kuingilia Uchaguzi Mkuu wa Marekani wa mwaka 2016, licha ya Trump kushtumu uchunguzi huo.

Chanzo:RFI

No comments:

Post a Comment