Wakenya wakipiga foleni kupiga kura mwaka 2017
Muungano mkuu wa upinzani nchini Kenya,
ambao ulishindwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, umeapa kuendelea na
maandamano wenye nia ya kubatilisha kile ambacho unasema kuwa, matokeo
"feki" ya uchaguzi mkuu.
Seneta James Orengo ameiambia BBC kuwa
chama chake, kinachoongozwa na Bwana Raila Odinga, hakitapinga matokeo
ya uchaguzi mkuu mahakamani, huku akisema kuwa Uhuru Kenyatta tayari
ametoa vitisho kwa majaji..
Kufikia sasa watu 11 wameuwawa katika
ghasia za baada ya uchaguzi mkuu, ambazo zilianza mara tu baada ya Uhuru
Kenyatta kushinda kutangazwa mshindi kwa muhula wa pili mnamo usiku wa
kuamkia Jumamosi.
Mpinzani wake mkuu Bwana Raila Odinga, amedai kuwa uchaguzi huo ulikubwa na wizi mkubwa wa kura.
Uhuru Kenyatta kushoto) na Mpinzani wake Raila Odinga (kulia)
Kaimu Waziri wa usalama wa ndani, Fred Matiangi, amewataja waandamanaji kama "wahalifu".
Kiongozi mmoja mkuu wa chama cha
uipinzani, Bwana Johnson Muthama, amesema kuwa, polisi wanajaribu
kuwalazimisha watu "wakubali matokeo hayo."
Tume ya kutetea haki za kibinadamnu
nchini Kenya, imetoa orodha ya juu ya wahasiriwa wa ghasia hizo huku
ikisema kuwa ni watu 24 ndio ambao wameuwawa katika visa vinavyohusiwa
na uchaguzi huo, huku ikiongeza kuwa polisi wanatumia nguvu kupita
kiasi.
Chanzo:BBC-SWAHILI
No comments:
Post a Comment