Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili,
Ali Hassan Mwinyi, akisikiliza maelezo kutoka kwa Inspekta Ibrahim
Samwix, wakati alipotembelea mabanda mbalimbali kwenye Tamasha la
Usalama Barabarani lililofanyika Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam. Kushoto
ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwenyekiti wa Baraza
la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili,
Ali Hassan Mwinyi (aliyevaa suti), akisikiliza maelezo jinsi uvunjaji wa
sheria za usalama barabarani unavyoweza kusababisha ajali, wakati
alipotembelea banda la Maaskari wa usalama barabarani, kwenye Tamasha la
Usalama Barabarani lililofanyika jana Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es
Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani,
Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akimkabidhi tuzo Mgeni Rasmi, Rais
Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, wakati wa Tamasha la
Usalama Barabarani lililofanyika jana Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es
Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo
wa Jeshi la Polisi, Nsato Marijani (kushoto), akipokea zawadi kutoka
kwa Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwenyekiti wa Baraza
la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni kwa niaba ya
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro kwa kutambua mchango
wake katika suala nzima la Usalama Barabarani wakati wa Tamasha la
Usalama Barabarani lililofanyika jana, Uwanja wa Uhuru jijini Dar es
Salaam.Kulia ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Balozi wa Usalama Barabarani,
Samira Abuu (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi,
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi na Naibu Waziri Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama
Barabarani,Mhandisi Hamad Masauni, baada ya kupokea cheti cha kutambua
mchango wake katika masuala ya Usalama Barabarani wakati wa Tamasha la
Usalama Barabarani lililofanyika jana, Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es
Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
No comments:
Post a Comment