Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo
amemuapisha Mhe. Benedict Martin Mashiba kuwa Balozi wa Tanzania nchini
Malawi
Mhe
Benedict Martin Mashiba amechukua nafasi ya Mhe. Victoria Richard
Mwakasege ambaye amestaafu nafasi hiyo, mbali na hilo Rais Magufuli
amepokea hati za utambulisho wa Mabalozi watano walioteuliwa
kuziwakilisha nchi zao hapa nchini.
Mbali
na hilo Rais Magufuli amewapongeza mabalozi hao kwa kuteuliwa
kuziwakilisha nchi zao hapa nchini na kuwaomba mabalozi hao kutilia
mkazo diplomasia ya Uchumi kwa kuongeza juhudi za kuhamasisha
wafanyabiashara na wadau wengine wa maendeleo kushirikiana na Tanzania
katika biashara na miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwepo ujenzi wa
viwanda, Kilimo na huduma za jamii.
Mabalozi waliowasilisha hati zao za utambulisho ni
1.Mhe. Nguyen Kim Doahn – Balozi wa Vietnam hapa nchini.
2.Mhe. Prof. Ratlan Pardede – Balozi wa Indonesia hapa nchini.
3.Mwadhama Askofu Mkuu Marek Solcynski–Balozi wa Vatican hapa nchini.
4.Mhe. Dkt. Detlef Wachter – Balozi wa Ujerumani hapa nchini.
No comments:
Post a Comment