Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na
Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani katikati (aliyevaa suti)
akimsikiliza Mkuu wa Kivuko/ Magogoni Kigamboni Mhandisi Lukombe
King’ombe wakati akimpa taarifa ndani ya chumba cha kuongozea kivuko cha
MV. KAZI alipotembelea kujionea utendaji kazi wake, wa kwanza kulia ni
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dk. Mussa Mgwatu .
Baadhi ya Wafanyakazi wa Wakala wa
Ufundi na Umeme (TEMESA) Makao makuu wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa
Wakala huo Dk. Mussa Mgwatu wakati akisoma taarifa fupi kwa Naibu Waziri
wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani aliyetembelea
ofisi za wakala huo kujionea utendaji kazi na kusikiliza changamoto
zinazoukabili wakala huo
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na
Umeme (TEMESA) Dk. Mussa Mgwatu katikati akitoa ufafanuzi wakati
alipokua akisoma taarifa ya wakala huo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi
Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani wa kwanza kushoto. Kulia
ni Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa wakala huo Hans Lyimo. Mheshimiwa
Ngonyani alitembelea ofisi za wakala huo kujionea utendaji kazi na
kusikiliza changamoto zinazoukabili wakala huo.
Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na
Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani katikati akimsikiliza Meneja wa
Karakana ya Mt Depot Mhandisi Moses Humbe wa kwanza kushoto alipokua
akimuelezea kuhusu utendaji kazi wa karakana hiyo. Kulia ni Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dk. Mussa Mgwatu.
Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na
Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani katikati mara baada ya kushuka
kutoka kivuko cha MV.KAZI alipotembelea kivuko hicho kukagua utendaji
kazi wake. Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme
(TEMESA) Dk. Mussa Mgwatu na kulia ni Mkuu wa Kivuko/ Magogoni Kigamboni
Mhandisi Lukombe King’ombe .
Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na
Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani katikati (aliyevaa suti) akipewa
ufafanuzi kuhusu eneo panapojengwa chumba kipya cha kukatia tiketi eneo
la Kigamboni na Mkuu wa Kivuko/ Magogoni Kigamboni Mhandisi Lukombe
King’ombe (wa pili kushoto aliyenyoosha mkono). Wa pili kulia ni
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dk. Mussa Mgwatu
anayesikiliza kwa makini.
Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na
Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani (wa pili kulia) akishuka kutoka
kwenye kivuko cha MV. KIGAMBONI mara baada ya kukagua utendaji kazi
wake, kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA)
Dk. Mussa Mgwatu.
No comments:
Post a Comment