Friday, August 18, 2017

MKUU WA WILAYA YA IKUNGI AZUNGUMZIA MICHUANO YA SOKA YA "IKUNGI ELIMU CUP" 2017

Mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Mhe.Miraji Mtaturu ametoa ufafanuzi kuhusiana na ligi ya "Ikungi Elimu Cup 2017" itakayozinduliwa kesho Agosti 19,2017 katika uwanja wa shule ya sekondari Ikungi wilayani humo.

Mhe.Mtaturu kaeleza sababu za kuanzishwa kwa ligi hiyo na namna itakavyosaidia kuhamasisha wananchi pamoja na wadau mbalimbali wa elimu katika kutatua changamoto za elimu wilayani Ikungi ikiwemo ujenzi wa madarasa, maabara pamoja na nyumba za waalimu kupitia mfuko wa elimu Ikungi ambapo yeye ni mlezi wa mfuko huo.
BMG Habari

No comments:

Post a Comment