Tuesday, August 8, 2017

TUMIENI UTAJIRI WA KOROSHO KUBADILISHA MAISHA YENU: MHE SAMIA SULUHU HASSAN

5
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia mkaa ulotengenezwa kutokana na makaratasi yaliotumika wakati alipotembelea banda la Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea wakati wa kilele cha sherehe ya maadhimisho ya 24 ya sikukuu ya Wakulima (Nane Nane) mkoani Lindi
6
Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhandisi Charles Tizeba akimuonesha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ubanguaji wa korosho wakati wa kilele cha sherehe ya maadhimisho ya 24 ya sikukuu ya Wakulima (Nane Nane) mkoani Lindi
7
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo juu ya magonjwa na wadudu wanaoshambulia mikorosho na namna ya kutibu mimea kutoka kwa Mtafiti  kiongozi wa Zao la Korosho wa Taasisi ya utafiti wa Kilimo Nahendele Bw.Fortunus Kapinga wakati  wa kilele cha sherehe ya maadhimisho ya 24 ya sikukuu ya Wakulima (Nane Nane) mkoani Lindi
8
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kushoto) akiwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Halima Ndendegu na Mkwe wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mama Salma Kikwete (MB) wakiangalia ufugaji wa samaki wa kwenye matenki unaofanywa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wakati wa kilele cha sherehe ya maadhimisho ya 24 ya sikukuu ya Wakulima (Nane Nane) mkoani Lind
9
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia karoti wakati alipotembelea na kujionea shughuli za kilimo cha mboga mboga zinazofanywa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wakati wa kilele cha sherehe ya maadhimisho ya 24 ya sikukuu ya Wakulima (Nane Nane) mkoani Lindi
10
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye kilele cha sherehe ya maadhimisho ya 24 ya sikukuu ya Wakulima (Nane Nane) mkoani Lindi.
2 
Sehemu ya wananchi waliohudhuria

Na Mathias Canal, Lindi 

Wakulima mkoani Lindi na Mtwara wametakiwa kutumia pesa za korosho walizopata katika msimu wa 2016/2017 kuboresha maisha yao pasina kutumia bila weledi.

Akihutubia mamia ya wakulima wafugaji na wavuvi waliohudhuria kufungwa kwa maadhimisho ya Nanenane 2017 Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu amewataka wananchi wa Lindi na Mtwara kutumia pesa walizopata kujenga makazi bora, kusomesha watoto na kununua chakula cha kutosha familia zao.

Aidha amewasifia wakulima hao kwa namna ambavyo wameweza kupokea  teknolojia za kilimo hivyo kubadilisha sura ya maonesho ikilinganishwa na maonesho ya mwaka jana.

Mhe Samia amemuagiza Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi kuhakikisha kuwa Wizara pamoja na Halamashauri kuhakikisha kuwa mfumo Mpya wa utolewaji was pembejeo unaboreshwa ili makosa yaliyojitokeza Mwaka Jana katika zao la korosho yasijirudie tena.


Alisema kuwa Serikali inatambua kuwa Mwaka Jana zao la korosho liliingizia Serikali fedha nyingi za kigeni hivyo Serikali haitaruhusu kwa namna yoyote uzembe utakaopelekea soko la zao hilo kushuka na hata mazao mengineJambo litakalosababisha Wananchi na Serikali kupoteza mapato.

Aidha, Makamu wa Rais Alisema kuwa anafahamu kuwa Wizara ya Kilimo imeanzisha mfumo was ununuzi wa Mbolea kwa pamoja yaaani (Bulk Procurement System-PBS) katika msimu wa 2017/2018 kwa kuqgiza aina mbili za Mbolea ambazo Ni Mbolea ya kupandia ya DAP na Mbolea ya kukuzia ya UREA.

Aliongeza kuwa serikali imekamilisha uhakiki wa madeni ya wazabuni was pembejeo ambapo hata hivyo hali sio nzuri kwani pembejeo zimefika Bilioni 38.

Kuhusu changamoto zinazowakabili Wananchi kuhusu Upatikanaji wa mitaji Alisema kuwa Serikali itaendelea kuhamasisha wazalishaji Kujiunga kwenye benki ya Maendeleo ya Kilimo pamoja na vyama vya akiba na mikopo SACCOS Ili kuweza kunufaika na fursa zinazoweza kupatikana Kutoka kwenye vyama hivyo.

No comments:

Post a Comment