Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili mjini Zanzibar jioni ya leo tayari kuhudhuria sherehe ya Siku ya Kizimkazi itakayoadhimishwa kesho tarehe 12 Agosti, 2017.
Akiwa katika Uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume, Makamu wa Rais amekutana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Bi. Patricia Scotland ambaye alikuwa safarini kuelekea Dar es Salaam.
Bi. Scotland alikuwa mjini Zanzibar kwa mazungumzo na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein.
No comments:
Post a Comment