Na Mathias Canal, Lindi
Kampuni ya East West Seed inasherekea miaka 35
tangu kuanzishwa kwake kwa kuonyesha mbegu bora za mazao ya mbogamboga katika
maonesho ya nanenane yanayofanyika Kitaifa katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
Akizungumza na mtandao wa www.wazo-huru.blogspot.com Msimamizi wa Matangazo na Mauzo wa kampuni hiyo Ndg Jimmy Masasi amesema kuwa kampuni hiyo imekusudia kumfikia kila mtanzania kwa kuwauzia mbegu bora na imara watanzania ili waweze kuzalisha mazao bora na yenye tija kwao na jamii kwa ujumla.
Alisema kuwa kampuni hiyo inauza mbegu za mazao ya mbogamboga na maua aina ya Mari Gold hivyo kupitia maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi wananchi watapata fursa ya kutambua na kufahamu zaidi kuhusu mbegu hizo.
Muonekano wa mazao ya mbogamboga yanayotokana na kampuni ya East West Seed katika eneo la banda la magereza Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi
Wakulima wa mazao ya mbogamboga wakiendelea kuzuru ili kupata elimu ya namna ya kulima mazao hayo Kwenye maonesho ya nanenane katika banda la kampuni ya East West Seed lililopo katika eneo la banda la magereza Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi
Muonekano wa mbegu za mazao ya mbogamboga zinazouzwa na kampuni ya East West Seed katika eneo la banda la magereza Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi
Msimamizi wa matangazo na mauzo wa Kampuni ya East West Seed Ndg Jimmy Masasi akiwa katika banda la kampuni hiyo lililopo katika eneo la banda la Magereza kwenye Maonesho ya nanenane Kitaifa yanayofanyika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi
Wakulima wa mazao ya mbogamboga wakiendelea kuzuru ili kupata elimu ya namna ya kulima mazao hayo katika banda la kampuni ya East West Seed lililopo katika eneo la banda la magereza Kwenye maonesho ya nanenane Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi
Wakulima wa mazao ya mbogamboga wakiendelea kuzuru ili kupata elimu ya namna ya kulima mazao hayo katika banda la kampuni ya East West Seed lililopo katika eneo la banda la magereza Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi
No comments:
Post a Comment