Monday, August 7, 2017

DKT TIZEBA: TUMEONDOA KODI ILI KUWANUFAISHA WAKULIMA WETU WA NDANI

Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mhe Dkt Dk Charles Tizeba akisisitiza jambo mara baada ya kutembelea banda la Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi wakati wa Maonesho ya Kilimo (Nanenane) yanayofanyika katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.

Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mhe Dkt Dk Charles Tizeba akiteta jambo na Waziri wa Kilimo Mifugo, Maliasili na Uvuvi Zanzibar Hamad Rashid Muhammed mara baada ya kutembelea banda la Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi wakati wa Maonesho ya Kilimo (Nanenane) yanayofanyika katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.

Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mhe Dkt Dk Charles Tizeba akiwasili katika banda la Ofisi ya Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi wakati wa Maonesho ya Kilimo (Nanenane) yanayofanyika katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.

Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mhe Dkt Dk Charles Tizeba akisisitiza jambo mara baada ya kutembelea banda la Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi wakati wa Maonesho ya Kilimo (Nanenane) yanayofanyika katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mhe Dkt Dk Charles Tizeba akisikiliza maelezo kuhu takwimu za hali ya chakula nchini mara baada ya kutembelea banda la Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, Kitengo cha uratibu wa mazao na taadhari ya awali wakati wa Maonesho ya Kilimo (Nanenane) yanayofanyika katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.

Na Mathias Canal, Lindi


Serikali imesema kuwa imefuta baadhi ya kodi na tozo ili kuwanufaisha wakulima wote  nchini ambao awali walikuwa wakilalamikia na kupinga tozo na kodi hizo kwa madai kuwa zilikuwa zikiwanyonya sio kuwakwamua na wimbi kubwa la umasikini.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mhe Dkt Dk Charles Tizeba wakati alipotembelea banda la Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi wakati wa Maonesho ya Kilimo (Nanenane) yanayofanyika katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.

Dkt Tizeba Alisema kuwa kwa muda mrefu serikali imekuwa ikipata malalamiko kutoka kwa wananchi mbalimbali hususani kwa wakulima nchini Tanzania wakipinga kodi na tozo mbalimbali zinazotozwa kwani zimekuwa zikiwanyonya badala ya kuwakwamua na wimbi kubwa la umasikini jambo ambalo serikali ililitazama na kuona umuhimu wake na hatimaye kufikia utekelezaji huo.


Ameyasema kuwa  hayo ya Nanenane ambayo Kitaifa yanafanyika Mkoani Lindi yenye kauli mbiu ya “Zalisha kwa Tija Mazao na Bidhaa za Kilimo Mifugo na Uvuvi ili kufikia Uchumi wa Kati” yanayofanyika yamedhamiria zaidi katika kumkwamua mkulima kutoka kwenye kilimo kwa ajili ya mahitaji ya ndani na kufikia hatua ya kilimo biashara.


Dkt Tizeba Alisema kuwa Jumla ya tozo 80 kati ya tozo 139 zimefutwa na tozo nne (4) zimepunguzwa viwango. Tozo, kodi na ada zinajumuisha  kufutwa kwa tozo kumi (10) na mbili (2) kupunguza viwango kwenye zao la tumbaku.  Kwenye zao la kahawa zimefutwa tozo 17 na moja (1) kupunguzwa kiwango; sukari zimefutwa 16; pamba tozo zilizofutwa ni mbili (2); kwenye korosho tozo mbili zimefutwa na chai imefutwa tozo moja (1).


Katika kuongeza upatikanaji wa pembejeo tozo tatu (3) zimefutwa na moja (1) imepunguzwa kiwango kwenye mbolea na  tozo saba (7) zilizokuwa kwenye mbegu nazo zimefutwa. Katika Ushirika jumla ya tozo 20 zimefutwa katika ngazi mbalimbali.


Katika Mifugo; kodi, ada na tozo saba (7) ambazo zilikuwa kero kwa Wafugaji, Wafanyabiashara na Wawekezaji nazo zilifutwa na kubakiza zile tu zenye uhusiano wa moja kwa moja katika uendelezaji wa Sekta ya Mifugo. Tozo zilizofutwa zinajumuisha mbili (2) kwenye maziwa; nyama tozo nne (4) na moja (1) kwenye afya ya mifugo.  


Katika Uvuvi, jumla ya kodi, ada na tozo tano (5) ambazo ni kero kwa Wavuvi, Wafugaji wa viumbe kwenye maji na wawekezaji nazo zimefutwa.


Serikali itaendelea kuchambua kwa kina tozo, ushuru na ada mbalimbali zilizobaki katika kilimo, mifugo na uvuvi kwa lengo la kuangalia uhalali wa kuwepo kwake ili kuwapunguzia wakulima, wafugaji na wavuvi mzigo wa tozo, ushuru na ada zisizokuwa na tija.


Dkt Tizeba alisema kuwa Hatua nyingine iliyochukuliwa ni ya kusamehe kodi ya ongezeko la thamani kwenye vyakula vya mifugo vinavyotengenezwa hapa nchini ili kupunguza gharama ya kununua chakula hicho kwa Wafugaji. Serikali pia, imesamehe kodi ya ongezeko la thamani kwenye mayai ya kutotoleshea vifaranga, lengo likiwa ni kupunguza gharama ya uzalishaji vifaranga na kukuza Sekta ndogo ya Ufugaji ili iweze kuongeza mchango katika Pato la Taifa.


Kuanzia msimu huu wa kilimo Wakulima wa korosho watapata bure pembejeo aina ya salfa zilizokuwa zikiuzwa kwa bei ya ruzuku Hatua hiyo ya utekelezaji wa azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ni  kuhakikisha kuwa vikwazo vyote vilivyokuwa vinawakabili wakulima wa zao la korosho vinaondolewa ili waongeze uzalishaji na tija zaidi kutokana na zao hilo. 
 
Dkt Tizeba ameongeza kuwa soko la chakula Tanzania ni moja hivyo wananchi wakiwa na uzalishaji wa kilimo chenye tija watanufaika na kukuza kipato cha mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.


MWISHO

No comments:

Post a Comment