NA Mathias Canal, Wazo Huru Blog
MKUU wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida Mhe Miraji Mtaturu amekutana na wadau wa mfuko wa elimu wilaya ili kuwahabarisha kuhusu kuanzishwa kwa Mfuko huo.
Akizungumza Wakati wa mkutano huo uliohudhuriwa na zaidi ya Wananchi 600 Mhe Mtaturu alisema kuwa wananchi sambamba na wadau hao wanapaswa kuwa wazalendo katika kutafuta njia za kutatua changamoto za elimu wilayani humo ikiwa Ni pamoja na kuchangia ili kuibua Mfuko huo.
Alisema kuwa kauli mbiu ya Mfuko huo itakuwa na dhamira ya Changia/Boresha Elimu Ikungi ambapo Mkuu huyo wa Wilaya Alisema Ikungi maendeleo inawezekana kwa Wananchi wenyewe kushirikiana na Serikali na kuwa na dhamira chanya ya kuimarisha Elimu.
Mfuko huo wa Elimu Wilaya ya Ikungi umeundwa baada ya uanzishwaji wake kuridhiwa na kikao cha baraza la madiwani kilichoketi hivi karibuni.
MTATURU Alisema kuwa mfuko huo utakuwa na jukumu la kuratibu masuala yote yatakayosaidia kuboresha utoaji wa elimu katika shule za msingi na sekondari.
Mtaturu alisema wakifanikiwa kuondoa changamoto zilizopo watakuwa wameboresha mazingira ya utoaji elimu na kuongeza ufaulu wa watoto jambo ambalo waliazimia walipokutana wadau wa elimu.
MWISHO
No comments:
Post a Comment