Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu akifanya moja ya mazoezi ya viungo pamoja na wananchi.
Sifa ya kiongozi ni kumsikiliza
mwananchi yoyote,wakati wote,mahali popote ikiwa ni pamoja na kutatua
kero na haja za wananchi ambayo ndio dhamira ya serikali ya awamu ya
tano,mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu analitimiza hilo pichani
akimsikiliza mmoja wa wananchi waliojumuika nae kufanya mazoezi.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji
Mtatutu akiwaongoza wakazi wa kata ya Makiungu na Mungaa katika jogging
ikiwa ni ufanyaji wa mazoezi ya viungo.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu akifanya moja ya mazoezi ya viungo pamoja na wananchi.
………………………………………………………………….
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji
Mtaturu ameshiriki kufanya mazoezi ya viungo na wananchi wa Kata ya
Makiungu na Mungaa zilizopo wilayani humo huku akitilia mkazo ufanyaji
wa mazoezi hayo sambamba na uzingatiaji wa ulaji wa vyakula visivyo na
mafuta mengi ili kuepukana na maradhi yasiyoambukiza.
Hatua hiyo ni kuunga mkono
maelekezo ya makamu wa Rais Samiah Suluhu Hassan ya kufanya mazoezi kila
jumamosi ya pili ya kila mwezi.
Akizungumza katika mazoezi hayo
Mtaturu amesema magonjwa yasiyoambukiza yamekuwa yakichukua maisha ya
watu wengi duniani hivyo ni wakati wa kuweka jitihada kupambana nayo.
“Mbali na kufanya mazoezi haya
kila mwezi lakini ni vizuri pia kuweka utaratibu wa kutembea walau mara
moja kwa siku iwe asubuhi au jioni lakini pia kuweka msisitizo kwenye
ulaji wa matunda na mboga za majani kwa wingi huku tukiepuka matumizi ya
mafuta mengi kwenye vyakula vyetu,”alisema Mtaturu.
Alisema rais John Magufuli
anasisitiza kauli mbiu yake ya hapa kazi tu na ili kauli mbiu hiyo iweze
kufanikiwa ni lazima tuwe na afya iliyo imara kwa kujenga tabia ya
kupima mara kwa mara na kufanya mazoezi.
“Ili kuweka mazoea ya ufanyaji wa
mazoezi tunapaswa tuanze kuwazoesha vijana wadogo na ili kutilia mkazo
hili hivi karibuni tutaanzisha ligi ya mpira wa miguu itakayoitwa Elimu
Cup ambayo itakashirikisha kata zote 28 wilayani hapa,”aliongeza mkuu
huyo.
Aliweka bayana lengo la kuanzisha
ligi hiyo kuwa ni kuhamasisha uchangiaji wa mfuko wa elimu na hapo
hapo kubaini vipaji vya vijana.
Kauli mbiu ya kuhamasisha mazoezi hayo ni mazoezi ni afya tokomeza magonjwa yasiyoambukizwa.
No comments:
Post a Comment