Shirika lisilo la Kiserikali la Culture and Development East Africa (CDEA) lenye makao makuu yake Mikocheni, Jijini Dar e Salaam, hivi karibuni limetoa mafunzo kwa wasanii wa muziki wanaochipukia kutoka Tanzania na Uganda, ikiwemo yale ya kinadharia na vitendo hasa katika Uandishi wa muziki na Elimu ya uongozi wa muziki ambapo mafunzo hayo yalitolewa kwenye kambi maalum ya siku tatu.
Akielezea kambi hiyo ya Wasanii wanaochipukia kutoka Afrika Mashariki, Afisa Mradi wa Atamishi ya Kazi za Sanaa CDEA, Bi Angela Kilusungu amebainisha kuwa kambi hiyo ilikuwa na mafanikio makubwa kwani anaamini Washiriki hao wameweza kupata maarifa ambayo yatasaidia vipaji vyao hasa kuviinua kutoka hatua moja hadi nyingine.
“Mfunzo haya yameandaliwa na mradi mkuba wa IIDEA,unaofadhilia na Shirika la GIZ EAC kwa lengo la kukutanisha wasanii wa Nchi mbalimbali za Afrika Mashariki kwa dhana ya ‘kuvuka boda’ na kuendeleza mshikamano wa Umoja wa nchi hizo katika kujitafutia nafasi ya kujiendeleza kifani,kutafuta masoko na mengineo.
Wasanii wachanga 18 walichaguliwa kushiriki kambi hiyo ya siku tatu iliyofanyika eneo la Eco Sanaa Terrace Mikocheni B jijini dar es salaam.
Washiriki walipata fursa kupitia matangazo tuliotoa kupitia mitandao ya kijamii kwa wasanii hao wachanga wa Uganda na hapa nchini na waliitikia wito na kujitokeza kwenye kambi hoyo” alisema Bi. Angela Kilusungu.
Na kuongeza kuwa: Wasanii hao walichaguliwa kutokana na vigezo vya uhitaji wa elimu ya biashara ya muziki na taaluma yalioainishwa kwenye baru pepe walizoandika washiriki” Bi Angela Kilusungu.
Mafunzo hayo yaliyongozwa na wakufunzi akiwemo Bi Natalie Likkenaer na Nelson Mandela Ambasa toka Chuo cha Stadi za muziki Sauti Academy, cha nchini Kenya ambacho ndicho kinachoongoza kwa kutoa wasanii maarufu wa muziki ukanda huu wa Afrika Mashariki na nchini Kenya wakiwem Bendi ya H_Art the Band ambao wanafanya vizuri kimuziki kwa sasa.
Washiriki Eileen Theodore na Kuchi wakifanya collabo jukwaani wakati wa tukio hilo la mafunzo hayo ya muziki
Pia wasanii hao waliweza kujengewa uwezo na wakufunzi mbalimbali wakiwemo Bi Prisner Nicholaus wa Mdundo Music mtaalamu wa masuala ya Biashara ya Muziki Matandaoni na Bi Azisa Ongala Muandaaji wa matamasha ya muziki hapa Nchini.
Bi Kilusungu alibainisha kuwa, Mafunzo yaliandaliwa kutoa taaluma ya kinadharia na vitendo katika nyadhfa mbalimbali ikiwemo Uandishi wa muziki uliotilia mkazo ushirikiano ‘Collabo’ na Elimu ya uongozi wa muziki, mpango mkakati wa muziki.
Pia waliweza kujifunza mbinu mbalimbali za kutumia jukwaa la muziki wa jukwaani yaani ‘live’.
Aidha mafunzo hayo pia yalitoa Nafasi kwa washiriki kujifunza biashara ya muziki mtandaoni na kutambua thamani ya matamasha mbalimbali ya muziki.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Sauti Academy, Bi Natalie Lukkenaer alibainisha kuwa:
“Tunategemea wanamuziki hawa watoke hapa na muswada wa nyimbo, mpango mkakati wa biashara zao na ujuzi wa kumiliki jukwaa kwa sababu ndiyo sehemu yao ya kuonesha uwezo wao kwenye suala zima la utumbuizaji” Alisema Bi Natalie Lukkenaer Mkurugenzi wa Sauti Academy.
Bi Natalie aliongeza kuwa, Muziki ni biashara kama biashara nyingine hivyo wasanii wachanga wanatakiwa kujitafutia Nafasi za kutoka nje ya mipaka yao wakia na utambuzi wa fani hiyo kibiashara zaidi na kusisitiza kuwa wanamuziki wanapaswa kuheshimu muziki kama taaluma iliyo rasmi na inaeza kulipa kodi husika za nchi na kujipatia kipato halali cha kujikimu.
Kuhusu suala la kuvuka mipaka Bi natalie aliwaasa sasanii wafikirie ushirikiano ama ‘collabo’ kwa wasanii wa chizi zaidi ya moja, kama njia mojawapo ya kuwawezesha kukamilisha lengo la wao kupata nafasi na wafuasi nchi ambazo wamelega kufikia kimasoko.
“Tunataka mazingira tulivu maeneo ya mipkani ili sisi wasanii tuweze kupita na vyombo vyetu na tupewe kipaumbele kwa maana muziki ni njia mojawapo ya kudumisha Amani na mshikamano baina ya watu”
Alisisitiza Mandela
Hata hivyo mwisho wa kambi hiyo, Wasanii walipata nafasi ya kutumbuiza nyimbo ambazo walizitunga siku ya ufunguzi wa mafunzo hayo kwenye jukwaa la Creatives Hook Up ambapo ni moja wapo ya miradi ya CDEA ambayo hutoa nafasi kwa wasanii kuonesha uwezo wao kitaaluma ama kifani.
Kambi hii ikiwa ni Muendelezo wa programu ya atamishi ya kazi za sanaa mradi ambao ulizinduliwa mwishoni mwa mwaka jana ujulikanao kama IIDEA, unaofadhilia na Shirika la GIZ EAC.
Bw. Madela Ambasa akisisitiza jambo wakati wa mafunzo
Washiriki La veda na Micku marvin Tz wakitumbuiza kwenye Creatives Hook Up
Mmoja wa washiriki Bi Sitenda kutoka Uganda, akionesha mfano kwa (wenzie Hawapo pichani)
Bi Aziza Ongala (aliyevaa kata mikono ya kijani) Akiwaelezea wasaniiKuhusu umuhimu wa matamasha
Bi Prisna Nicholaus akiwaelezea Jambo wasanii
Bw. Mandela Ambasa Akiwaelekeza wasanii wa muziki kuhusu Hisia
Bi Angela kilusungu Afisa Mradi wa Atamishi ya kazi za sanaa akiongelea jambo wakati kambi hiyo ya kuwapika wanamuziki chipukizi
Wakufunzi Bi natalie na Bw. Mandela Ambasa wa Suti Academy wakiwaelekeza wanamuziki kuhusu jukwaa
Msanii Hamis Cholo akifurahia Cheti cha Ushiriki alichotunukiwa baada ya mafunzo
Washiriki wa kambi ya wanamuziki wakimsikiliza mwalimu (hayupo pichani)
Washirki Allen Soul Tz Jaka Mukiga na Bennysofar Tz wakijifunza kutumia jukwaa kwa kushirikiana
No comments:
Post a Comment