Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(Takukuru) iwakamate watendaji 12 wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya
wakiwamo aliyekuwa mstahiki meya Athanas Kapuga.
Amesema
pia wakamatwe, wakurugenzi watatu, kaimu mkurugenzi, wahasibu wawili na
wajumbe wa bodi wanne kwa kuisababishia hasara jiji hilo kiasi cha Sh63
bilioni katika ujenzi wa Soko la Mwanjelwa.
Amewataka
makamanda wa Takukuru kuanzia leo wawakamate watuhumiwa hao na kwamba
anatuma timu kutoka ofisi ya waziri mkuu kwa ajili ya kuandaa mashtaka
hayo ambapo itatua Mbeya Jumatano.
No comments:
Post a Comment