Na Mwandishi wetu kutoka Zanzibar
Mkutano mkuu wa umoja wa vijana wa CCM wadi ya Kwahani umefanyika leo katika tawi la CCM Kwaalamsha.
Mgeni rasmin wa uchaguzi huo MH Miraji Kwanza Muakilishi wa CCM jimbo la Chumbuni ( *MNEC*) alisema siku ya leo ni siku muhimu sana kwake maana yeye binafsi ni umoja wa vijana umemtoa mbali sana.
Vijana leo mnagombea nafasi za wadi kesho mtagombea nafasi kubwa sana kuliko hizi ndani chama na ndani ya serekali ata Mimi niliazia nafasi ya katibu hamasa tawi 1991 nikaendalea nafasi mbali mbali mpaka nikawa Mwenyekiti UVCCM Mkoa wa Kaskazini nikawa *MNEC* hatimae leo ni Mwakilishi.
Hayo yote yamekuja baada ya kuwa na subira na bidii ya kujitolea ndani ya Chama nakuombeni muwe na subira na mjitolee kwenye chama mtafanikiwa alisema MH Miraji Kwanza.
Mwisho mgeni rasmin Mh Miraji aliwaasa vijana wasichaguwe kiongozi ambae atakuwa wa Mbunge au Muwakilishi wachguwe viongozi ambao watakuwa wao ili awatumikie vijana baada ya nasaha hizo MH Miraji alifungua rasmin mkutano huo na kuwatakia kila la kheri wajumbe na wagombea wote.
No comments:
Post a Comment