Kumekuwepo
na upotoshaji wa mafunzo ya utarajali (Internaship programme) bila
malipo yaani fedha za kujikimu wakati wa mafunzo hayo kwa baadhi ya
wanaotarajia kuanza mafunzo kwa vitendo mapema mwaka huu.
Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inapenda
kuwajulisha kwamba kwa sasa hakuna ‘intern’ aliyepangiwa kuanza mafunzo
hayo kwani tunasubiri watoke waliopo kwenye mafunzo.
Barua
iliyodukuliwa na kusambaa kwa lengo la kupotosha wataraji hao ilikuwa
ni kwa ajili ya wataraji (intern) kutoka nje ya nchi ambao kwa sheria
hawalipiwi na Serikali ya Tanzania.
Aidha
wapo ‘intern’ wawili ambao wanasoma nchini China na mwingine Algeria
masomo yao yalihitaji mafunzo kwa vitendo kabla ya kumaliza na kwa kuwa
ilikua lazima warudi vyuoni mwezi Oktoba waliomba kufanya mafunzo hayo
kwa kujigharimia pamoja na kuwa ni watanzania na wazazi wao walikuwa
wameridhia hilo kwa maandishi ili warudi mapema kumalizia program yao
ya udaktari.
Hivyo
ni watanzania wawili tu wameshapata barua yenye kuwataka kujilipia kwa
mazingira hayo hakuna wengine waliyepewa barua ya kuruhusiwa kwenda
mafunzo ya utarajali (internship) bila malipo.
Imetolewa na;
Nsachris Mwamwaja
Mkuu Kitengo cha Mawasiliano Serikali-Afya
30/7/2017
No comments:
Post a Comment