Mashindano ya Mbio za Baiskeli katika Mikoa mitano ya Kanda ya ziwa yanataraji kufanyika AGOSTI 6, 2017 katika Viwanja vya Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mkoani Simiyu.
Mashindano hayo yameandaliwa na Kampuni ya uzalishaji wa Vinywaji Baridi ya JAMBO FOOD PRODUCT kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.
Mashindano hayo yatahusisha Umbali wa Kilomita 200 kwa Wanaume, Kilomita 80 kwa Wanawake na Kilomita 5 kwa watu wenye Ulemavu.
Pia kutakuwa na Burudani Mbalimbali Kutoka kwa WAGIKA na WAGARO na Ngoma nyingine nyingi za Asili zitatolewa siku hiyo. Zawadi Mbalimbali zitatolewa kwa washiriki ikiwemo Pikipiki na fedha Taslimu zaidi ya Shilingi Milioni nane.
Fomu za Ushiriki wa SIMIYU JAMBO FESTIVAL 2017 zinapatikana katika Ofisi za Maafisa Michezo katika Halmashauri za Mikoa ya Simiyu, Shinyanga, Mwanza, Mara na Geita kwa Gharama ya Shilingi 5000 tu.
Mgeni rasmi Katika Mashindano hayo ya mbio za Baiskeli ya SIMIYU JAMBO FESTIVAL 2017 atakuwa ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Tulia Ackson Tulia.
Mkoa wa Simiyu, Wilaya Moja Bidhaa Moja
HAKUNA KIINGILIO KATIKA MASHINDANO HAYO, NYOTE MNAKARIBISHWA
No comments:
Post a Comment