Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Comred Shaka Hamdu Shaka amevutiwa na Kasi ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi inayofanywa na Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula kwa kushirikiana na Madiwani wake.
Kaimu Katibu Mkuu huyo ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kuitembelea na kuikagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa kwa wananchi ndani ya Jimbo la Ilemela ikiwemo Utoaji wa Mikopo kwa Vijana na wakina Mama, Mradi wa Ufyatuaji wa Matofali unaotekelezwa na Taasisi ya The Angeline Foundation kwa kushirikiana na Manispaa ya Ilemela kwa ufadhili wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC na Mradi wa Kilimo cha Kisasa ambapo amesema
‘Niseme tu hakika unaitendea haki nafasi yako ya Ubunge ambayo wenzio wana Ilemela wamekuamini lakini unatupa matumaini kuwa Jimbo hili hakuna sababu ya kutoka ndani ya mikono ya Chama Cha Mapinduzi litaendelea kuwa chini ya mwanamama ambae ni kama mwanababa akiwa mbele katika kuendesha mapambano, Nitoe wito kwa wabunge wote nchini hasa wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi kuiga mfano wa Dkt Angeline Mabula pamoja na majukumu yake ya kitaifa amekuwa hakauki Jimboni’
Aidha Katibu Shaka amewaasa wananchi na viongozi wa wilaya ya Ilemela kuendelea kumuunga mkono Mbunge huyo katika kuwaletea wananchi maendeleo kama mabavyo kauli mbiu ya wilaya hiyo inavyosema ya ‘Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga’
Kwa upande wake Mbunge wa Ilemela Dkt Angeline Mabula mbali na kumshukuru Kaimu Katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi kwa kutembelea shughuli mbalimbali za maendeleo zinazotekelezwa ndani ya Jimbo lake amemuhakikishia kuwa Ilemela itaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo kama Ilani ya Chama Cha Mapinduzi inavyoelekeza sambamba kuwa kimbilio la wananchi wanyonge kwa kuwatetea
Ziara hiyo pia ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa chama hicho kwa Ngazi ya wilaya na Mkoa wa Mwanza pamoja na Madiwani Manispaa ya Ilemela
‘Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga’
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
16.07.2017
No comments:
Post a Comment