Na Wazo Huru Blog, Ukerewe-Mwanza
Umoja Wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa umesema kuwa pamoja na changamoto mbalimbali ambazo zinaendelea kupatiwa ufumbuzi na serikali ya Awamu ya tano lakini Chama Cha Mapinduzi (CCM) Pekee ndicho kitakachowaletea wananchi maendeleo ya Kijamii, Kiuchumi na Kisiasa hivyo wananchi wanapaswa kuendelea Kukiunga mkono.
Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) Leo Julai 23, 2017 Wilayani Ukerewe Mkoani Mwanza Wakati wa ziara ya siku moja alipokuwa akizungumza na Vijana wa Jumuiya ya Chama hicho (UVCCM) pamoja na wanachama wa chama cha Mapinduzi (CCM) katika Mji wa Nansio Wilayani humo.
Shaka alisema kuwa kila unapomalizika uchaguzi Mkuu wananchi wanapaswa kushughulika na shughuli za kijamii ili kukuza uchumi wao na Taifa kwa ujumla hivyo wanapaswa kuweka kando itikadi za kisiasa.
"Huu ni muda wa kuungana na Rais katika kuhakikisha nchi inasonga Mbele kijamii na kiuchumi, Itikadi za kidini, Kisiasa na kikabila zinapaswa kuwekwa kando kwa maslahi mapana ya Taifa" Alisema Shaka
Alisema kuwa Vijana na watanzania kwa ujumla wake wanapaswa kujituma kwa kufanya kazi kwa bidii ili kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli za kuwaletea maendeleo wananchi.
Alisema kuwa Vijana wanapaswa kuanzisha vikundi vya ujasiriamali, na Vikundi vya uzalishaji Mali, Vitakavyowasaidia Vijana, Wanawake na Taifa kwa ujumla kupambana na hali ya kiuchumi katika jamii.
"Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa Mhe Dkt John Pombe Magufuli anatuhimiza kufanya kazi kwa bidii na hivyo ili kupambana vizuri katika hali zetu kiuchumi ni wazi kuwa lazima tukubali kuweka siasa kando" Alisema Shaka
Awali Kaimu Katibu Mkuu huyo alizindua mashina ya wakereketwa Tawi la Kakukuru Kijijini Murutilima na kuzindua Shina la Wakereketwa eneo la Kitanga katika Kata ya Kakukuru.
Katika Hatua nyingine Shaka alisema kuwa wananchi wote wanapaswa kutendewa haki kwa kupatiwa Huduma bora katika kila eneo.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment