Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula leo amepokea Ugeni wa wadau wa maendeleo kutoka nchini Korea ikiwa ni muendelezo wa jitihada zake katika kuwaletea wananchi wa jimbo lake maendeleo
Akizungumza mara baada ya kuupokea ugeni huo Dkt Angeline Mabula amewahakikishia wageni hao ushirikiano huku akiasa viongozi na wananchi kuunga mkono jitihada hizo za kutafuta wadau wa maendeleo kutoka ndani na nje ya nchi lengo ni kujiletea maendeleo ya haraka na yenye tija kwa vizazi vya sasa na baade
‘… Niwaombe wananchi wote na viongozi wenzangu kuhakikisha tunatoa ushirikiano kwa wenzetu hawa kutoka Youngnum University nchini Korea walioungana nasi katika kuhakikisha tunapata maendeleo ya haraka …’ Alisema
Ugeni huo unataraji kuzuru maeneo mbalimbali hapo kesho sambamba na kuzungumza na viongozi wa wilaya ya Ilemela na Mkoa wa Mwanza kwa ujumla wake kufanikisha adhma yao ya kumuunga mkono Mhe Dkt Angeline Mabula katika kuwatumikia na kuwaletea maendeleo wananchi wake wa Jimbo la Ilemela kabla ya kuelekea kijiji cha Ihalalo kata ya Sangabuye Manispaa ya Ilemela unapotekelezwa mradi wa kijiji cha mfano
‘Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga ’
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
30.07.2017
No comments:
Post a Comment