Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mhe Rosemary Staki Senyamule amekamilisha ziara ya uhamasishaji wa wanachi kujiunga na Mfuko wa BIMA ya Afya CHIF.
ZIARA hiyo ya ukamilisho wa uhamasishaji imefanyika Leo katika kata ya Ndungu Na Kihurio kwa kutoa eliku juu ya umuhimu wa kujiunga na Mfuko huo.
Aidha Mambo muhimu yaliyohimizwa katika uhamasishaji ni pamoja na Wajibu wa wananchi Kuhakikisha wanajiunga kwa kwa Wakati kama yalivyo makubaliano ambao wengi wao ni kati ya mwezo Agosti Na mwezi Saptemba mwishoni na Kutoa taarifa za watumishi ambao hawafuati maelekezo ya Huduma zilizoahidiwa kwenye CHIF.
Kwa upande wa Wajibu wa viongozi WDC Na halmashauri za Vijiji ni Kujiunga Na CHIF kabla ya Tarehe 1/08/2017 kwa wote wasio Na Bima ya Afya, Kuhamasisha Na kuhakikisha kata zote zinajiunga Na CHIF yaani Nyumba kwa nyumba, Kusimamia ubora wa Huduma zinazotolewa kwenye vituo vyote. Mfano Kadi ya CHIF kwanza, Dawa kuwepo Na ziagizwe kwa wakati, sambamba na lugha nzuri.
Sambamba na hiyo pia Kujifanyia tathmini Mara kwa mara Hususani kila mwezi, ili kujua mwenendo kama mwenendo itakuwa na mafanikio zaidi ama laa sambamba Na kufanya mageuzi haraka inapokuwa vinginevyo.
Pia Wajibu wa wafanyakazi ni Kutoa Huduma zote na kwa wakati kama zilivyoahidiwa kwenye miongozo ya CHIF.
Mwisho ni wajibu wa Halmashauri sambamba na NHIF ni Kuendelea kutoa motisha kwa wafanyakazi wanaofanya vizuri Na kuchukua hatua kwa wasiofanya vizuri, Ufuatiliaji wa Karibu wa Huduma, upatikanaji wa dawa, kufanya malipo kwa wakati kwa kila kituo, tathmini Na kuchukua hatua haraka.
No comments:
Post a Comment