Mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi amewashauri wakulima wa mahindi kuongeza kwa thamani kwa kusaga mahindi ili kuzalisha unga.
Chumi alitoa ushauri huo baada ya kutembelea ghala la mahindi ya Kikundi cha uzalishaji wa mahindi kinachoongozwa na Mwanamama Vicky Ng'umbi.
'Tunatarajia kuvuna takribani magunia elfu nane, lakini hatujui kwa kuuza mana tunasikia kuwa serikali imezuia kuuza mahindi nje ya nchi' alifafanua Mama huyo mjasiriamali.
Akifafanua Chumi, alisema ni faida zaidi kusaga unga kuliko kuuza mahindi.
'Ushauri wangu, kwa uwezo mdogo mlionao msisite kusaga mahindi na kuzalisha unga, itawapa faida ya unga, pumba mnaweza kuwauzia watu wenye mifugo wakazalisha chakula cha mifugo'
Mbunge huyo aliongeza kuwa tujifunze katika sekta ya mazao ya misitu ambapo badala ya kuuza magogo, wanapasua mbao.
Mbunge huyo aliwatembelea wakulima hao wakati akikagua shughuli za maendeleo ikiwemo ujenzi wa chumba cha upasuaji ambao ni ufadhili wa msaada wa fedha za Japan.
Aidha Chumi, alitembelea ujenzi wa shule ya msingi Gangilonga ambapo ibahitajija shilingi milioni nne na laki tisa kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa choo cha Walimu.
Katika kuhakikisha kuwa shule hiyo inapokea wanafunzi kama ilivyopangwa, Chumi alitoa shilingi milioni mbili kutoka ofisi yake.
Mbunge huyo pia alikagua ujenzi wa barabara ya Changarawe -Bumilayinga na ujenzi wa tanki la maji la lita laki tano linalojengwa Kinyanambo.
Miradi mingine ni pamoja na ujenzi wa karavati la barabara ya Bafanabafana kwenda Lumwago na ukamilishaji wa Zahanati ya Ulole ambayo Mbunge huyo pia ameahidi kutoa shilingi milioni mbili ili kusaidia ifunguliwe.
No comments:
Post a Comment