Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema msimamo wa Serikali wa kuzuia usafirishaji wa chakula kwenda nje ya nchi uko pale pale.
Waziri
Mkuu ametoa kauli hiyo jana Alhamisi Juni 29, 2017 Bungeni mjini
Dodoma wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu
wakati akijibu swali la Ritha Kabati (Viti Maalumu) aliyetaka ufafanuzi
kuhusu zuio la kusafirisha mazao nje ya nchi kwa mikoa yenye chakula
cha ziada.
“Tumedhibiti
na kuzuia usafirishaji wa chakula hasa mahindi kwenda nje ya nchi ili
kuliepusha Taifa kukumbwa na baa la njaa kutokana na baadhi ya mikoa
kutopata mavuno ya kutosha,
“Kuna
maeneo kama ya Sengerema na Geita mahindi yamekauka, hivyo bado tuna
upungufu wa chakula. Na hata bei ya chakula ipo juu, hatuna namna
nyingine zaidi ya kudhibiti utokaji wa chakula kwenda nje na nawasihi
wananchi tushirikiane katika jambo hili,” alisema.
Waziri
Mkuu alisema kama kuna ulazima wa kusafirisha chakula kwenda nje ya
nchi wahusika wakaombe kibali kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
na kibali kiwe cha kusafirisha unga na si mahindi.
"Nimeeleza sisi tumedhibiti kutoa mahindi nje bila ya kibali na kama kuna umuhimu wa kuyapeleka mahindi nje basi yasagwe ndani ili upelekwe 'unga' maana ukisaga kuna faida zake, pumba tunazitumia kwa chakula cha mifugo lakini pia mashine zetu tunazo sisitiza viwanda zitapata kazi ya kusaga pamoja na kutoa ajira" alisisitizia Majaliwa.

No comments:
Post a Comment