Waandamanaji wakipinga agizo la Donald
Trump linalopiga marufuku raia kutoka nchi sita za Kiislamu kuingi
Marekani, Januari 29, 2017 Washington DC.
Sheria ya rais wa Marekani kuhusu
uhamiaji na usafiri kwenda Marekani kwa raia kutoka nchi sita za
Kiislamu imeanza kutekelezwa leo Ijumaa saa sita usiku (00:00). Kwa sasa
raia kutoka mataifa hayo sita ya Kiislamu na wakimbizi wote
wanakabiliwa na masharti magumu ya kuingia nchini Marekani.
Kulinagana na sheria hii mpya ya usafiri
nchini Marekani, Bibi, shangazi, mjomba, binamu na mpwa hawakubaliki
kuwa watu wenye uhusiano wa karibu na mtu anayetaka kuingia taifa hilo.
Sheria hii inamaanisha kwamba watu wasio
na uhusiano wa karibu na wale wanaoishi nchini Marekani ama uhusiano wa
kibiashara nchini Marekani huenda wakanyimwa visa na kuzuiliwa kuingia
nchini humo.
Kwa mujibu wa sheria hiyo mpya, katika
kipindi cha siku 90 zijazo raia kutoka mataifa hayo sita wasio na
uhusiano wa karibu na raia wa Marekani hawataruhusiwa kuingia nchini
humo.
Kulingana na sheria hii mpya, Wale walio
na Visa hawataathiriwa.Wale wenye uraia wa mataifa mawili wanaotumia
pasipoti zao pia wataruhusiwa.
Awali Jimbo la Hawaii liilishutumu serikali ya Marekani kwa kukiuka sheria ya mahakama ya juu kupitia kuwatenga watu.
Mapema juma hili, mahakama ya juu ilikubali sheria ya Trump kuhusu usafiri kutumika kwa muda.
Mahakama iliamuru kwamba watu
wanaotafuta visa kuingia Marekani kutoka mataifa sita ya Kiislamu pamoja
na wakimbizi wote, watalazimika kuthibitisha kuwa na uhusiano wa karibu
na raia wa taifa hilo.
Mahakama ya juu inatarajiwa kutoa uamuzi wa mwisho kuhusu marufuku hiyo mnamo mwezi Oktoba mwaka huu.
RFI
No comments:
Post a Comment