Na Tiganya Vincent-RS-Tabora
WADAU wa zao la tumbaku kutoka Tabora
na Katavi wametakiwa kusaidia wakulima wa zao hilo kuendelea na kilimo
hicho bila kuharibu mistu iliyopo kwa ajili ya kuyaepusha maeneo hayo
kuwa katika tishio la kuwa jangwa.
Kauli
hiyo imetolewa jana mjini hapa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey
Mwanri wakati akifungua mkutano wa siku wa wadau kutoka mikoa ya Tabora
na Katavi.
Madhumuni
ya mkutano huo ilikuwa ni kujadiliana ili kuja ya mpango wa kumsaidia
mkulima wa tumbaku kuendelea na kilimo hicho huku akiwa na mipango
endelevu ya utunzaji wa mistu.
Alisema
kuwa mipango hiyo ni pamoja na kila mkulima kuwa na takwimu sahihi ya
kuni zinazohitajika kwa mwaka katika ukaushaji wa zao lao ili ziendane
na mipango ya upandaji wa miti mipya kwa wakulima hao katika maeneo yao.
Bw.
Mwanri aliongeza kuwa mipango mingine ni pamoja na kuwaelimisha juu ya
ujenzi wa majiko ya kisasa ya ukaushaji wa tumbaku ambayo mkulima
anatumia matawi ya miti badala ya magogo ambacho ndio chanzo kikuu cha
uharibifu wa mistu.
Kwa
upande wa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga
alisema kuwa wakulima wa tumbaku katika eneo lake wamejitahidi kutumia
majiko ya kisasa ambayo kwa kiasi kikubwa yamezuia ukataji ovyo wa
mistu.
Alisema
kuwa tatizo kubwa linalowakabili wao ni uvamizi wa makundi makubwa ya
mifugo kutoka mikoa jirani ambapo inakadiriwa kuwepo na zaidi ya ng’ombe
milioni 3 na hivyo kuvamia maeneo mbalimbali ya mistu na hifadhi.
Mkuu
huyo wa Mkoa wa Katavi alisema katika kukabiliana na tatizo hilo tayari
wameshaondoa zaidi ya ng’ombe elfu 40 walikuwa wamevamia katika maeneo
ya wilaya ya Tanganyika.
Meja
Jenereali Mstaafu Muhuga aliongeza kuwa zoezi hilo la kuyaondoa makundi
ya ng’ombe linatarajia kuendelea mwezi Julai mwaka huu.
Naye
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Tumbaku Tanzania Louis Roussos aliwaomba
wadau kuwasaidia wakulima kuwa na mbinu mbadala ya kuendesha kilimo cha
tumbaku kuwa kwa kuhakikisha kuwa mistu inakuwa endelevu.
Alisema
kuwa kinyume cha hapo tumbaku ya Tanzania ipo hatarini kukataliwa na
Kampuni kubwa duniani kwa sababu haziko tayari kununua zao ambalo
linasababisha uharibifu wa mazingira.
Bw.
Roussos aliongeza kuwa ni vema wadau wakatumia fursa hiyo kuhakikisha
wanapata mikakati ya kuwasaidia wakulima wa tumbaku waendelee kunufaika
na tumbaku huku wakitunza mistu.
No comments:
Post a Comment