Waziri
wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba jana ‘alimkalia kooni’ Mbunge wa
Arusha Mjini, Godbles Lema (Chadema) kwa kauli yake kwamba wabunge
wanaogopa kujadili mauaji yanayoendelea Kibiti wakihofia yatahamia kwao.
Mwigulu
alichukizwa na kauli hiyo jana bungeni wakati wa mjadala kuhusu
kuridhia itifaki ya udhibiti wa mazingira ya bahari na ukanda wa Pwani
ya Magharibi ya Bahari ya Hindi kutokana na vyanzo na shughuli
zinazofanyika nchi kavu.
Nyingine ni itifaki ya Kusimamia Upatikanaji na Mgawanyo sahihi wa faida zinazotokana na matumizi ya rasimali za jenetiki.
Wakati akichangia, Lema alisema wabunge wasishangae mauaji yanayotokea Kibiti yakisambaa nchi nzima.
“Kila mtu anaogopa kujadili suala la Kibiti, Bunge linaogopa kujadili wanaona wakianza kujadili jamaa anaweza kuhamia huku,”alisema Lema.
Akijibu, Waziri Mwigulu pamoja na mambo mengine, alisema Serikali haitaacha eneo hata moja la nchi likatawaliwe na wahalifu.
“Tutashughulika na mmoja mmoja, watu wetu watafanya kazi katika mazingira salama.
“Unaongea
kimzaha mzaha, taswira iliyoko ndani inahusiana na siasa, leo
ukituambia yale ya Kibiti yanaendelea na maeneo mengine tunaendelea
kutafuta uhusiano, kama leo kauawa wa CCM, kaacha mwingine kule…. kuna
haja ya kutusaidia kwa nini unasema yanaendelea, kwa nini unadhani
wanashindwa…
“Katika
panga kazi zetu tunahakikisha wananchi wa maeneo yote wanakuwa
salama…sentesi kama hizi hata kama zinasemwa bungeni nadhani kuna
umuhimu ndugu zetu hawa wakasaidia kujua kiini ama kinatoka bungeni
ama kinatoka wapi, lakini sasa wanahangaika na watu wengine,” alisema.
Wilaya
za Mkoa wa Pwani za Rufiji, Kibiti na Mkuranga zimekumbwa na mauaji ya
viongozi wa vijiji na vitongoji tangu Mei mwaka jana na hadi sasa
zaidi ya watu 30 wameuawa.
Mauaji
mengi yamekuwa yakifanyika usiku kwenye nyumba za viongozi na watu
wengine ambao wamewahi kushika uongozi, idara ya maliasili na polisi.
Bunge
jana liliridhia itifaki ya udhibiti wa mazingira ya Bahari na Ukanda wa
Pwani ya Magharibi ya Bahari ya Hindi kutokana na vyanzo na shughuli
zinazofanyika nchi kavu na ile ya itifaki ya Kusimamia Upatikanaji na
Mgawanyo sahihi wa faida zinazotokana na matumizi ya rasimali za
jenetiki.
No comments:
Post a Comment