Na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es salaam Mhe Kisare Makori ameamuru kuwekwa kizuizini kwa masaa 48 Mweka hazina wa Kikundi Cha ulinzi shirikishi Mtaa wa Msewe Kata ya Ubungo Ndg Raymond Mlimba kwa kushindwa kuonyesha vielelezo vya matumizi ya fedha alizopewa kupeleka Benki.
Agizo Hilo limetolewa wakati wa Mkutano wa Mkuu wa Wilaya na wananchi wa Mtaa huo Mara baada ya kumtaka Mweka hazina huyo kutoa majibu kuhusu matumizi ya fedha zilizotakiwa kuwekwa Bank kwa ajili ya malipo ya vijana wanaounda umoja wa kikundi Cha ulinzi shirikishi.
Kutokea kwa kadhia hiyo kulijili Mara baada ya Kila mwananchi aliyesimama kuzungumza kulalamikia matukio ya uhalifu hususani wizi ambayo yameanza kutokea mara kwa mara katika mtaa huo mara baada ya vijana waliokuwa wakishiriki kwenye ulinzi shirikishi kutolipwa fedha zao kwa mujibu wa makubaliano.
Mweka Hazina huyo alishindwa kuonyesha vielelezo vya uwekaji na utoaji wa fedha Bank ambapo aliwaeleza wananchi mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo kuwa amehifadhi jumla ya shilingi milioni 1.2 ilihali Fedha zilizotajwa na Ofisa Mtendaji wa Mtaa zilizopo Bank ni Shilingi laki sita pekee.
Mhe Makori pia amemuagiza Mwenyekiti wa Mtaa wa Msewe kuitisha mkutano wa Mtaa ili kufanya makubaliano ya kuunda kamati ya Ulinzi shirikishi kwani hiyo ni njia rahisi ya kukomesha matukio ya ukabaji na uporaji ambayo yameshamiri kutokana na umbali wa vituo vya Polisi.
Mhe Makori amepokea maombi mengine ya wananchi hususani Ujenzi wa Kituo Cha Polisi, Kero ya maji machafu, Ombi la Zahanati ya Msewe kupandishwa hadhi na kuwa Kituo Cha afya, Sambamba na Ombi la kuboreshwa madarasa ya shule ya Msingi Msewe na mazingira yake ambapo ameahidi kuyatolea majibu hivi karibuni.
Alisema kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Mhe Dkt John Pombe Magufuli inadhughulika na kuwatetea wanyonge kwa kusikiliza kero zao na kuzitatua sambamba na kusukuma gurudumu la maendeleo kwa watanzania wote pasina kujali itikadi ya vyama vyao ama dini zao.
Ziara ya Mkuu wa Wilaya Mhe Kisare Makori ni muendelezo wa kuzuru katika Mitaa ya Wilaya ya Ubungo ili kuwafikia wananchi mahali walipo na kuzitambua changamoto zinazowakabili ili kuzipatia ufumbuzi.
IMETOLEWA NA;
OFISI YA MKUU WA WILAYA YA UBUNGOMkuu wa Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es salaam Mhe Kisare Makori akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Msewe Kata ya Ubungo kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya shule ya Msingi Msewe.Ofisa Mtendaji wa Kata ya Ubungo Ndg Isihaka Waziri akizungumza wakati wa mkutano wa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori uliofanyika viwanja vya shule ya Msingi Msewe.Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es salaam Mhe Kisare Makori akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Msewe Kata ya Ubungo kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya shule ya Msingi Msewe.Mwenyekiti wa Mtaa wa Msewe, Kata ya Ubungo Ndg Idan Fransis Msuya akizungumza wakati wa mkutano wa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori uliofanyika viwanja vya shule ya Msingi Msewe.Baadhi ya wananchi wa Mtaa wa Msewe, Kata ya Ubungo wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori wakati akihutubia Mkutano uliofanyika viwanja vya shule ya Msingi Msewe.Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori (Katikati), Ofisa Tarafa ya Kibamba Ndg Beatrice Mbawala (Kushoto) na Mwenyekiti wa Mtaa wa Msewe (Kulia) Ndg Idan Fransis Msuya Wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya shule ya Msingi MseweOfisa Tarafa ya Kibamba Ndg Beatrice Mbawala akisisitiza Jambo kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori kuhutubia Mkutano uliofanyika viwanja vya shule ya Msingi Msewe.Bi Manase Msajigwa Konongwa Mkazi wa Mtaa wa Golani akieleza kadhia ya wizi iliyowahi kumkumba hivi karibuni mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya shule ya Msingi Msewe, Kata ya UbungoBi Mariam Makubi Mkazi wa Mtaa wa Msewe akieleza kero yake mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya shule ya Msingi Msewe Kata ya Ubungo.Baadhi ya wakazi wa Mtaa wa Msewe Kata ya Ubungo wakimlaki Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es salaam Mhe Kisare Makori mara baada ya Mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya shule ya Msingi Msewe kumalizika.Baadhi ya wakazi wa Mtaa wa Msewe Kata ya Ubungo wakimlaki Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es salaam Mhe Kisare Makori mara baada ya Mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya shule ya Msingi Msewe kumalizika.
No comments:
Post a Comment